November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miaka 30,jela kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

Na Stephen Noel- Mpwapwa

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi mfawidhi ya wilaya ya mpwapwa mkoni DODOMA imewahukumu kifungo cha
miaka (30) gerezani mtu mmoja aliye fahamika kwa jina Mohammed Shaban Mawanja kwa kupatikana na hatia ya unyanga’nyi kwa kutumia silaha na kumuachilia huru bwana Leonsi Winston Lusito kwa kushidwa kupatikana Katika hatia iliyo kuwa inamkabili.

Kesi hiyo namba 27 ya mwaka 2022 iliyokuwa inamkabiri , Mohammed Shaban Mawanja na Leonsi Winston Lusito ambapo waliiba pikipiki aina ya Haujio yenye usajili namba MC164 CMN Mali ya Abdalah Jumanne ambae ni dreva Boda boda imetolewa hukumu na Hakimu mkazi mfawidhi Nuruperdesia Nassary.

Akiiambia Mahakama, Hakimu Mwendesha wa Polisi,Michael Joseph kuwa tukio lilitokea April 4. 2021 ambapo bwana Mawanja alikodisha bwana Abdalah Jumanne ili ampeleke kijiji cha Inzomvu na ndipo walipofika huku kwa KUTUMIA kipande cha nondo alipiga mhanga huyoo na kumrjeruhi na kumpora pikipiki.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua muda muda wa dakika 54Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Nuruperdesia Nassary alisema mshitakiwa alipatikana na hatia kufutia
Kifungu cha sheria namba na 287(A)ya kanuni ya adahabu sura 16 iliyofanyiwa malejeomwaka 2019

“Mshitakiwa amepatikana na hatia kwa mujibu wa kifungu
287(A) cha kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa malelejeo mwaka 2019
inayo inayo eleza unayangajnyi wa kutumia siraha”ameeleza Nassary

Kabla ya mahakama hiyo haijatoa hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka wa
Polisi Michael Joseph ameiomba Mahakama itoe adahabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwao kwa watu wengine kama wao ambao hawapendi kujishughulisha na kutumia njia za mkato katika kutafuta mali na utajiri.

Katika utetezi wake mtuhumiwa ameiomba
Mahakama imuachilie huru kwa sababu hati ya hati ya mashitaka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria kama maelezo ya kosa hayakujitosheleza kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa kifungu cha 132, na kifungu cha 135 na maelekezo ya sheria na polisi (PGO) namba 229.

Akimsomea hukunu hiyo hakimu Nassary alisema mahakama imemtia
hatiani kwenda kutumikia kifungu jela kwa miaka 30.

Na alidai ambae hakuridhika na maamuzi hayo anaweza kukata rufaa ndani ya Siku thelathini.