Na Esther Macha,Timesmajira Online,Mbeya
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mc Luvanda branding Entertainment ,Edwin Luvanda ameiambia Timesmajira online leo Aprili 21,2023 kuwa wanatarajia kufanya sherehe hizo maarufu kama Usiku wa Muungano Aprili 26 mwaka huu katika mji wa Tunduma Mkoa wa Songwe.
“Sherehe za Muungano zitakutanisha watu wa aina mbalimbali wakiwepo Wakurugenzi, wakuu wa Wilaya,watumishi ,wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na wananchi ambazo ni maalum kwa ajili ya kuwaenzi wahasisi wetu akiwepo Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Amani Abeid Karume ”amesema.
Luvanda amesema kuwa kupitia sherehe hizo wanatarajia wageni kutoka nchi za jirani za Zambia na Malawi watajifunza tamaduni za Tanzania sambamba na amani iliyopo ambayo itawakutanisha viongozi pamoja hususani wa kisiasa ,kidini na serikali.
Amesema siku ya usiku wa Muungano umeratibiwa na kampuni ya Luvanda Branding Entertainment kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Tunduma na kwamba wafanyabishara watumie fursa hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki.
Naye Mratibu wa usiku wa Muungano ,Furaha Mapunda amesema kuwa kati ya washiriki 1,300 wanatarajia 150 kutoka nchi jirani ya Zambia ambapo watagawanyiia katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza watu 1,000 watashiriki mchana huku 300 usiku.
“Tumetenga makundi mawili kwa sababu maalum ikiwepo watu 1,000 watashiriki mambo mbalimbali hususan mpira wa miguu,pete,kukimbiza kuku,kuvuta kamba na masuala ya mila na desturi ambazo zitaonesha picha na taswira nzuri kwa wageni,”amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya Luvanda Branding Entertainment,Daudi Shubata amesema lengo la kuandaa sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuenzi utamaduni uliaochwa na wahasisi wa Tanu akiwepo Hayati Mwalimu Nyerere na Amani Abeid Karume.
“Ujio wa wageni kutoka nje ya nchi ni jambo la kujivunia kwani watakuja kujifunza namna Watanzania wanavyoishi ,kunywa,kula pamoja na viongozi pasipo kujali itijkadi za udini,ukabila wala uchama,”amesema.
Ofisa Elimu Mkoa wa Songwe ,Michael Lugola amesema kitendo cha kufanyika sherehe za muungano katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma ni heshima kubwa sambamba na kufungua milango ya kiuchumi kwa wafanyabishara.
“Ni jambo la kujivunia sana kwani tunatarajia kupokea ugeni kutoka nchi jirani za Malawi na Zambia na viongozi wakubwa kutoka mikoa mbalimbali wakiwepo wa chama na Serikali hivyo niwatake wananchi kutumia fursa hiyo katika ushiriki ”amesema Lugola.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa