Na Mwandishi wetu, timesmajira
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Songwe, Fatuma Hussein amewatoa hofu vijana kutokana na serikali kusitisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 iliyokuwa ikitolewa katika ngazi za Halmashauri.
Mwenyekiti Fatuma ameyasema hayo leo katika Ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Songwe ambapo amesema kuwa kama UVCCM wanaamini kuwa serikali itakuja na mpango bora zaidi wa utoaji wa mikopo.
Amevitaka vikundi ambavyo vilikwisha undwa kuendelea kujiandaa na pindi dirisha la mikopo litakapozinduliwa wawe wa kwanza kunufaika na fedha hizo.
Aidha katika hatua nyingine Fatuma ameiomba serikali kuharikisha ujenzi wa soko la Tunduma ambalo lipo katika hatua za mwisho kwani wananchi wengi wanasubiri kwa hamu soko hilo ambalo litakuwa ndio mkombozi wa vijana wengi kujiajiri.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â