Judith Ferdinand, Mwanza
Watu wawili wamefariki baada ya kuliwa na mamba kwa nyakati tofauti katika Ziwa Victoria wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP.Wilbrod Mutafungwa, ameeleza katika tukio liliilotokea Machi 24,2023 majira ya saa 1(19:00) jioni huko mwalo wa Kazunzu, kijiji na Kata ya Kazunzu, katika fukwe za ziwa Victoria kuliripotiwa taarifa ya mtu kuliwa mamba.
Baada ya taarifa hiyo Askari Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifika eneo hilo ambapo ndugu waliweza kuutambua mwili wa mtu aliyekamatwa na kuliwa na mamba kuwa ni Salome Dotto mwenyewe umri wa miaka 30,mkazi wa Kazunzu.
Ambapo Kamanda huyo ameeleza kuwa mwili huo umefanyiwa uchunguzi naa daktari na tayari umekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.
Huku tukio jingine liliilotokea Machi 9,2023 majira ya  saa 7 (13:00) huko kijiji cha Izindabo, kata na tarafa ya Buchosa Wilaya ya sengerema, kuliripotiwa taarifa ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Primitiva Evarist mwenyewe umri wa miaka 56, mkazi wa Izindabo.
Mtu huyo alifariki baada ya kukamatwa na kuliwa na mamba wakati akinawa miguu katika fukwe za ziwa victoria.
Ambapo mwili wa Primitiva Evarist ulitambuliwa na ndugu na kufanyiwa uchunguzi kisha kukabidhiwa kwa taratibu za mazishi.
Jeshi hilo limwaasa wananchi hususani wanaofanya shughuli zao katika fukwe za Ziwa Victoria kuchukua tahadhari ya usalama wao wenyewe ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria