NA MWAINDISHI WETU, MOROGORO
KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Public Accounts Committee-PAC)
imeipongeza Serikali kwa kuridhia uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Mradi wa Uendelezaji wa shamba
(Rachi) ya kunenepesha Mifugo na Machinjio ya kisasa wa Nguru Hills Ranch
ulioko Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Pongezi
hizo zimetolewa baada ya wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Makamu
Mwenyekiti wa PAC Japhet Hasunga kutembelea kiwanda hicho kwa nia ya kukagua
uwekezaji uliofanywa na PSSSF kwenye Mradi huo.
“Kamati
yetu ni kuangalia thamani ya fedha, matumizi ya fedha, hivyo tuna wajibu wa kuhakikisha
hizo fedha kama kweli zimetumika na uwekezaji wake una tija, niwapongeze kwa
uwekezaji huu, ukiangalia manufaa ya kiwanda kwa jamii inayozunguka eneo hili, ajira, kwakweli ni mafanikio ya utekelezaji wa
Ilani ya CCM.” Alifafanua Mhe. Hasunga.
Mradi
wa Machinjio ya Nguru Hills unaendeshwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kushirikiana na Wabia wenza ambao ni Kampuni ya
Eclipse Investiment LLC na Kampuni ya Busara Investment LLP
Akizunguzma mara baada ya kutembelea Mradi huo Mjumbe wa Kamati Mhe.
Issack Kamwelwe aliipongeza PSSSF kwa uamuzi wa kuingia ubia na wawekezaji wa nje.
“Huu
ni mfano mzuri kwa wengine na muutangaze, Arabuni huwezi kwenda kuwekeza bila ya kuwa na
mwenyeji wa pale, hapa nchini kuna baadhi ya wawekezaji wamewekeza bila ya kuwa na
Mtanzania ndani ya uwekezaji huo, niwapongeze sana PSSSF kwa kutoka na kuungana na wawekezaji wa nje.” Alipongeza Mhe. Kamwelwe.
Alisema kazi kubwa iliyo mbele ni kutangaza kwenye soko (marketing).
“Kwa ubora wa
nyama tuliyoiona hapa, mimi makazi yangu ni Morogoro, Dar es Salaam na Dodoma
tuelekezane ili na mimi nianze kutumia nyama ya kutoka hapa.” Alisema Mhe.
Kamwelwe.
Akiwakaribisha
wajumbe wa Kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini PSSSF, Dkt. Aggrey Mlimuka alisema Machinjio ya Nguru
Hills hutumia malighafi kutoka kwa wafugaji walioko wilaya ya Mvomero na maeneo
jirani
Alisema
Kiwanda hununua Ng’ombe kutoka kwa wafugaji, kisha hukaa nao kwa muda ili
kuwanenepesha kufikia kiwango kinachohitajika.
“Ng’ombe
wa chini ya Kilo 300 hachinjwi na akinunuliwa lazima atunzwe kwa nia ya kumnenepesha
hadi afikie kiwango hicho.” Alisema.
Alisema
wao kama Bodi wajibu wao mkubwa ni kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa kwa
usimamizi madhubuti katika kiwanda hicho.
Akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa Mradi, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema, PSSSF
iliungana na wabia wengine mwaka 2017
ikimiliki hisa asilimia 39% huku wabia wengine wawili wakimiliki jumla ya asilimia 61%.
Alisema
Mradi huo unajumuisha Ranchi ya Mifugo pamoja na Machinjio ambapo eneo lote
lina ukubwa wa Hekta 2328 sawa na Mita za Mraba Milioni 23, 280,000 ikiwa na uwezo wa kutunza Ng’ombe elfu 10,000 na Mbuzi 15,000 kwa wakati mmoja.
Alisema
Machinjio hayo yana eneo la Jengo la kiwanda (Utawala), machinjio, eneo la
kufungashia (Packeging), maabara, eneo lamkubadilishia nguo na vyumba vya
kupozea (cold rooms) na visima vine vikubwa vyenye uwezo wa kuzalisha lita 20,000
kwa saa.
Alisema
kwa siku kiwanda kinachinja Ng’ombe 100 kwa siku na Mbuzi 1,000 kwa siku.
“Mpaka
sasa kiwanda kimezalisha tani 150 za nyama sawa na N’ombe 1,153 zenye thamani
ya shilingi Bilioni 1.59, tuko kwenye hatua za kukamilisha kupata kibali cha
1S0-220000 ili tuwe na uwezo wa kusafirisha nyama kwenye nchi ambazo zinahitaji
hati ya ubora ya ukaguzi ubora ISO.” Alifafanua CPA. Kashimba.
Alisema
manufaa ya uwekezaji ni kuongeza thamani ya Mfuko kutokana na mapato
yatakayotokana na uwekezaji, kuongeza kipato cha wafugaji na wakulima, kuongeza
pato la taifa lakini pia kuongeza ubora wa bidhaa za ngozi.
Alisema
kampuni ya Nguru Hills Rach inatumia mawakala kukusanya Ng’ombe kutoka kwa
wafugaji lakini pia wafugaji moja kwa moja wanaweza kuleta mifugo yao lengo ni
kuhakikisha mali ghafi (Ng’omba na Mbuzi) zinapatikana wakati wote.
Alisema
Bidhaa zinazozalishwa zinazingatia viwango vya kimataifa kwa kufuata taratibu
za HACCP (Hazard Analysis and Critical Control Points) na kwa kufuata misingi
ya halal.
Lengo
la Kampuni ya Nguru ni kuuza asilimia 80 ya bidhaa zake nje ya nchi na asilimia
20 katika soko la ndani ya nchi.
“Tayari
tumepokea oda ya kupeleka nyama iliyogandishwa
tani 54 kwa wiki kwenye nchi za UAE, kwa hivyo tutakapopata tu ISO .”
Alibainisha CPA.
Alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita, kuna mabadiliko makubwa ya kisera yaliyopelekea mazingira mazuri ya uwekezaji.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini PSSSF, Dkt. Aggrey Mlimuka (kushoto) Mkurugenzi Mkuu PSSSF, CPA. Hosea Kashimba na Meneja Uhusiano na Elimu Kwa Umma wa Mfuko huo, James Mlowe wakiwasubiri kuwapokea wageni wao (Wajumbe wa Kamati ya Bunge PAC)
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi