November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mahundi:wanawake CCM Mbeya waahidi kumpa kura za kishindo Rais Samia 2025

Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi.Maryprisca Mahundi amesema kupitia Umoja wa Wanawake CCM Mkoa wa Mbeya wamejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu 2025 Rais Samia Suluhu Hassan anapata kura za kishindo.

Mhandisi Mahundi ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya , amesema hayo katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya kwenye sherehe za kumpongeza Rais Samia kwa kutimiza miaka miwili tangu ashike madaraka baada ya kufariki mtangulizi wake Dkt,John Magufuli.

Amesema wapo kwenye nafasi yakuhakikisha kura za kishindo kwa Rais Samia kutokana na mambo makubwa aliyoelekeza mkoani hapo katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwepo huduma ya maji na kumtua mama ndoo kichwani.

‘’Kwa dhamana yangu kama Naibu Waziri wa Maji tunamshukuru Rais Samia kwa kuwatua ndoo kichwani ,msimamo wetu tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja, wanawake tutaacha kutembea umbali mrefu kutafuta maji….,maji yanatusogelea kwenye makazi yetu lengo kubwa ni siye kujizatiti kwenye shughuli za kiuchumi ,”amesema Mahundi na kuongeza kuwa

“Kwa sasa tunaenda kufanya biashara kwenye masoko,kulima,kufungua maduka tutakuwa na shughuli mbali mbali ambazo zitajumuishakwenye uchumi wa kila mmoja’’amesema Mhandisi Mshindi.

Pia amesema Rais ameongeza huduma yaupatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 6.8,ambapo wakati anaingia madarakani mwaka 2021 maji yalipatikana kwaasilimia 70.1 ilipofika Desemba 2022 tayari kuna maji asilimia 76.9.

Mbunge wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Bahati Ndingo, amesema kuwa wanatambua miaka miwili ya Rais Samia amefanya mambo makubwa hususani sekta ya kilimo imeongezeka mara mbili zaidi tangu uhuru pamoja na sekta ya afya.

Naibu waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza katika kongamano hilo la kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika vya shule ya msingi Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya.
Baadhi ya vijana wa hamasa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya wakipita na mabango katika siku maalum ya kumpokeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili ya Uongozi wake.