Na Lubango Mleka, Igunga.
WAKULIMA wa Skimu ya Umwagiliaji zao la Mpunga katika kijiji cha Mwanzugi, Kata ya Igunga, Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora wametakiwa kufuata ratiba waliyopewa ya mgao wa maji katika mashamba yao.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala wilaya ya Igunga bwana Godslove Kawiche kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Sauda Mtondo baada ya kupatiwa ushauri na wataalamu wa kilimo na umwagiliaji kutokana na mabadiriko ya tabia nchi yaliyopelekea kukosekana kwa mvua za kutosha ambazo zingelijaza bwawa la umwagiliaji katika skimu hiyo.
” Tunajua sote msimu wa kilimo cha mpunga huwa tunaanza mwezi wa 11 kwa kuandaa mashamba kwa kusia mbegu na mwezi wa 12 mpaka wa kwanza mwanzoni huwa tunapanda, kwa hiyo mtaona kwamba tumechelewa kwa sababu ya kiwango cha maji kinachopaswa kifunguliwe hakikufika kutokana na tatizo ukame,” amesema Kawiche.
Ameendelea kusema kuwa kwa mkoa wa Tabora wenye wilaya saba, wilaya ya Igunga ndiyo haikupata mvua za uhakika kutokana na mabadiriko ya tabia nchi yaliyotokana na wananchi kukata miti hovyo jambo lililopelekea kuathili hali ya hewa na kupelekea ukame.
“Ili kuepukana na changamoto hii kunakampeni tunaanzisha ya upandaji miti kuanzi shuleni kila mwanafunzi apande mti na autunza, lakini pia kwenye taasisi, Vituo vya Afya, Zahanati, Mahakama, Ofisi za Serikali, Vijiji, Tarafa, Kata, mtu mmoja mmoja na kwafamilia tunakwenda kupanda miti ili kuondokana na mabadiriko ya tabia nchi, wataalamu wamasema kuwa kuanzia wiki hii mvua zitaanza kunyesha basi wote tuliopo hapa tujipange kwenda kupanda miti,” amesema Kawiche.
Kawiche amesema kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ilikaa na wataalamu na kuwaelekeza kukitembelea chanzo cha maji na bwawa na kuona nini kifanyike ambapo wataalamu hao walitoa ushauri nini kifanyike kutokana na kina cha maji katika bwawa hilo kuwa kidogo.
“Tulitegemea kiwango cha maji kingeongezeka kufikia ujazo wa mita 6.5, kwa wale mliotembelea bwawa mmeona kiwango cha maji kiko mita 4 na hatuna uhakika kama mvua zitakazo nyesha zitafikisha ujazo wa kiwango cha 6.5, kwa hiyo ushauri tuliopewa na wataalamu kuwa maji yaliyopo yaanze kutumika kwa shamba la ndani ambalo ni shamba la ushirika,” amesema Kawiche.
“Hatuna uhakika hata haya maji yaliyopo kama yataivisha kwa mpunga, tumuombe Mungu hizi mvua zinazonyesha zijaze bwawa, kwani wataalamu wametuambia kuwa ni asilimia 70 tu ndio watakao ivisha na asilimia 30 hatuna uhakika nao, tumefanya hivyo kwa sababu huu ni mwaka wa njaa, bora tupate kidogo kuliko tukakosa kabisa.”
Aidha amesema kuwa, wameweka utaratibu wa kugawa maji hayo kwa zamu, na itaandaliwa ratiba ambayo itabandikwa katika ofisi ya Ushirika, ofisi zote za Serikali, ambapo amewaomba watu wote wenye mashamba kufuata ratiba hiyo na kuhudumia mashamba yao kwa saa 24.
“Tumekubaliana kuunda kikosi kazi kitakacho fuatilia ratiba hii, hatuwezi kuwaacha ushirika peke yao, itakuwa na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vitakavyo ratibu zamu kwani mitalo ipo mitatu, itakuwa maji yanagaiwa siku mbili na mtalo wa mwisho utapata sikutatu, zamu itakayofuata ule uliopata siku mbili nao utapata siku tatu, kwa hiyo tutakuwa tunazunguka,” amesema Kawiche.
Katika hatua nyingine Kawiche, amewataka wakulima kununua mbolea ya ruzuku na kuitumia kama ilivyo kusudiwa na si kuiuza kwa watu wengine ambao hawajajisajili kwani kuna wakala ambao wameteuliwa kwa kazi hiyo na si vinginevyo.
Amesema kuwa atakaye hujumu ratiba hiyo atachukuliwa sheria, pia maji hayo yatafunguliwa kwa siku 165 badala ya siku 155, ambapo yatafunguliwa kuanzia Machi 20 na kufungwa Agosti 3,12023.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Usirika na Umwagiliaji Mwamapuli, Ramadhan Muna amewataka wakulima hao kuzingatia maagizo waliyopewa, na kushirikiana na kikosi kazi kilichoundwa kufichua watu au kikundi cha watu watako hujumu miundombinu ya maji na Umwagiliaji ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wao wakulima wa eneo hilo Rashid Jumanne Kayanda, wameipongeza Serikali kwa kuchukua uamuzi huo na kuruhusi maji kufunguliwa katika mashamba yao, na kuahidi kufuata utaratibu wa zamu ya kumwagilia maji mashamba yao kama ulivyowekwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo na Ushirika.
“Mimi nimepokea kwa furaha sana tamko hili na yale yote yaliyoongewa katika kikao hiki na Mkuu wa Wilaya, ninategemea haya maneno aliyoyaongea yawe ya uhakika, maana yake kunatatizo moja la watu wenye mashamba ya nje kubomoa njia za maji na kuyaiba kwenda kwenye mashamba yao, kwa kuwa ametuhakikishia vyombo vya ulinzi na usalama vitashirikiana na sisi wakulima tutashukuru sana, na tumuombe Mwenyezi Mungu mvua zinyeshe ili tuepukane na janga la njaa,” amesema Kayanda.
Huku William Bwiriza amesema kuwa, watafuata ratiba na kulima kwa wakati ili kwendana na ratiba hiyo huku kusisitiza wananchi kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi