November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

wahimizwa kutunza mazingira na fukwe ziwa victoria

Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Kutunza mazingira ni wajibu wa kila mwananchi,hivyo jamii imehimizwa kuhakikisha inatimiza wajibu huo,kwa kutunza mazingira ya maeneo yao pamoja na  fukwe za Ziwa Victoria.

Ambapo utunzaji wa mazingira unasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi,kujikinga na magonjwa ya mlipuko na kuwa na mandhari mazuri ya kuvutia watalii.

Wito huo umetolewa na  Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam shule ya Sayansi na Teknolojia ya Uvuvi,Bahati Mayoma wakati wa zoezi la kufanya usafi na utoaji wa elimu juu ya kutunza mazingira na urejeshaji wa taka ngumu katika mialo ya Halmashauri ya  Manispaa ya Ilemela.

Ambapo,amewaekeza wananchi  kuhakikisha hakuna uingizaji wa plastiki ndani ya ziwa hilo, utekelezaji wa shughuli za kibinadamu kando ya vyanzo vya maji.

Bahati pia amezihimiza BMU kusimamia wajibu wake ikiwemo usafi wa ziwa na mazingira yake pamoja na kubainisha tafiti mbalimbali zinazoelezea juu ya namna Ziwa Victoria na mazalia yake vinavyoathiriwa na uharibu wa mazingira.

Kwa upande wake, Ofisa Mazingira wa Halmashauri ya  Manispaa ya Ilemela  Jonathan Nyabugumba,amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kusafisha maeneo yao wanayoishi.

Pia  kutunza mazingira yanayowazunguka ili kujikinga na magonjwa yanayosababishwa na uchaguzi wa mazingira kama vile kipindupindu na magonjwa ya tumbo.

Ambapo ameeleza kuwa ni wajibu wa  wananchi kuyatunza mazingira siyo  mpaka  wasimamiwe na Serikali huku akiwasisitiza mawakala wa usafi kutekeleza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi.

“Nawashukuru wadau wa mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, Arena recycling na Emedo ya jijini Mwanza,wananchi endeleeni  na utamaduni wa kufanya usafi hata baada ya taasisi hizi zinazotoa elimu ya mazingira kumaliza muda wao wa kazi ndani ya Ilemela,”ameeleza Jonathan.

Wavuvi wa mwalo wa Igombe Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela mkoani Mwanza, wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam kwa kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali za EMEDO na NORCE mara baada ya zoezi la kufanya usafi wa mwalo huo, kupata Elimu ya utunzaji wa mazingira na urejeshaji taka ngumu.
Wataalam wa utunzaji wa mazingira na urejeshaji taka ngumu kutoka taasisi za EMEDO na NORCE wakionyesha namna ya kutenganisha taka kwaajili ya zoezi la urejeshaji.
Mtaalam wa Mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam,Bahati Mayoma,akitoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira na fukwe kwa wavuvi wa Mwalo wa Igombe, wilayani Ilemela mkoani Mwanza hawapo pichani.