Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline, Dodoma.
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limewataka vijana nchini kuwa makini na matapeli kwani kumekuwa na tabia ya kuibuka matapeli pindi matangazo ya nafasi za kujiunga na jeshi hilo zinapotangazwa.
Kauli hiyo imetolewa jijini hapa leo,Machi 9 ,2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na uhusiano wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda ,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya nafasi za kujiunga na Jeshi kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidato cha nne hadi shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba wa mafunzo ya kujitolea JKT na kurudishwa majumbani.”Natambua katika matangazo haya ya kujiunga na nafasi hizi kuna matapeli watajitokeza na kuanza kupenyeza utapeli wao ,mara jaza fomu hii kitu ambacho siyo kweli hivyo nawataka watanzania wasidanganyike wala kurubuniwa na hakuna njia ya mkato katika kupata nafasi hizi zaidi ya kuzingatia vigezo vilivywekwa wazi kabisa,
“Mtambue kwamba Matapeli ni Binadamu hivyo kutokana na kukua kwa teknolojia kila siku wanabuni mbinu mpya hivyo inabidi kuchukua tahadhari kwa pamoja ili kuepukana na mitego ya utapeli wao,”amesema Luteni Kanali Ilonda
Aidha Luteni Kanali Ilonda amesema nafasi hizo zinawahusu vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu.
“Nafasi hizi haziwahusu vijana ambao bado wapo katika kambi mbalimbali za JKT kwa sasa bali zinawahusu wale ambao tayari wamemaliza mikataba yao ya mafunzo ya miaka miwili na kurudishwa majumbani na wenye vigezo vilivyotajwa vya kuomba nafasi hii,” amesisitiza Luteni Kanali Ilonda
Aidha,Luteni Kanali Ilonda, ametaja vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa maombi hayo kuwa mwombaji awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na akili timamu,awe na cheti halisi cha kuzaliwa,vyeti vya shule nav yeti vya taaluma.
Vigezo vingine ni pamojana na awe hajatumikia Jeshi la Polisi,magereza,Chuo cha Mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo na asiwe ameoa au kuolewa.
Pamoja na hayo ameeleza utaratibu wa jinsi ya kutuma maombi ambapo amesema kuwa maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya jeshi hilo Dodoma kwanzia leo Machi ,9 hadi Machi 20, 2023 yakiwa na viambatanisho kama vile nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya nida,nakala ya cheti cha kuzaliwa,vyeti vya shule na chuo,nakala cheti cha JKT na namba ya simu ya mkononi ya muombaji na maombi yanaweza kutumwa Kupitia njia ya barua pepe ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi