January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Unastahili uhakika na usalama wa chombo chako kila unapokuwa barabarani

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kwa kuendelea kuwajali na kuwathamini Watanzania, Benki ya NMB ikishirikiana na makampuni ya Bima, inatoa huduma ya bima ya gari au chombo cha moto kwa lengo la kutoa kinga dhidi ya hasara itokanayo na ajali, wizi, uharibifu na majeraha ya mwili/ kifo kwa mtu mwingine.

Ukikata bima na NMB, wamerahisisha njia ya kutoa taarifa ya ajali, huku wakihakikisha wanafuatilia na kukupa maendeleo ya madai yako ili uyapate kwa muda mfupi sana.

Unachohitaji ni;
·         Nakala ya kadi ya chombo na kitambulisho halali
·         Picha za chombo kwa wakati huo
·         Thamani ya chombo

Tembelea tawi lolote la NMB karibu yako ukate bima ya gari sasa!

TelezaNaHii #Umebima #NMBKaribuYako