Na Mwandishi wetu,Arusha
WANAFUNZI wa Chuo Cha Nelson Mandela African Institute of Science and Technology (NM-AIST) kampasi ya jijini Arusha,wamepatiwa mafunzo ya siku sita ya ushauri juu ya muonekana mzuri wa bidhaa na ubora wa bidhaa.
Kambi hiyo ilifanyika juzi mkoani humo yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi kuandaa
mkakati wa wazi wa uuzaji na utangazaji wa bidhaa na huduma zao ambapo Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Sahara Ventures ili kuwawezesha wanafunzi hao kupata ujuzi wa kutosha .
Akizungumza na vyombo vya habari,Mwezeshaji wa Mafunzo hayo,Idrisa Jaffary amesema mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa wanafunzi mbinu bora na njia sahihi wanazoweza kuzifuata
kuongeza mwonekano wa haraka na kuboresha uaminifu wa watumiaji kwa bidhaa zao.
Alisema mbali na Mafunzo hayo, dhana nyingine, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela walichojifunza ni kuhusu uwasilishaji na zana za mawasiliano kwa wanaoanza.
“Nilipata fursa ya kuwafundisha juu ya kuongeza muonekano mzuri wa bidhaa na uuzaji kama moja ya mipango yangu
kuelimisha watu juu ya dhana hizi mbili, jinsi na wakati wa kutumia kila moja,” alisema
mwezeshaji,”alisema na kuongeza
“Kutokana na uzoefu wangu wa kufanya kazi katika wakala wa ubunifu na uboreshaji wa bidhaa kama mtaalamu wa mikakati anayefanya kazi moja kwa moja jambo ambalo linawavutia wateja wengi,”amesema
“Mwaka huu ninachukua mtazamo mpana zaidi kwa wanafunzi hao ambao ni vyuo Cha kufanya dijitali kamili kwa kuunda yaliyomo
sauti (Podcast) na video ambazo zinashughulikia sana utangazaji na uuzaji na kutengeneza
mafunzo yanapatikana kwa urahisi kwa wote,” amesema
More Stories
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua