November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Askari kata watakiwa kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online, Kilimanjaro

JESHI la Polisi limesema kuwa lilianzisha mkakati wa Polisi kata likiwa na dhamira ya kushirikiana na watendaji wa kata kwa kutafuta taarifa za uhalifu na kuzifanyia kazi katika maeneo yao ikiwa ni Pamoja na kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijnsia.

Kauli hiyo imetolewa leo Januari 26 na kamishina wa Polisi kamishine ya Polisi jamii CP FAUSTINE SHILOGILE wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Kilimanjaro,wakaguzi kata Pamoja na watendaji wa kata ambapo amesema Jeshi hilo limesema kuwa liliweka utaratibu huo ili kujenga jamii yenye mawazo mapya juu ya utendaji wa Jeshi hilo kupitia Polisi kata.

Aidha Jeshi hilolimesema lilihakikisha kuwa Tanzania bara na visiwani kuna kuwa na askari kata ambae atashirikiana na watendaji wa kata kuhakisha jamii ya eneo husika inaishi kwa amani na utulivu kwa kutafuta taarifa za uhalifu na wahalifu katika kata husika.

CP Shilogile ameeleza kuwa Jeshi hilo lilimeweka utaratibu huo ikiwa ni sehemu ya kuweka ukaribu wa askari wa Jeshi hilo na wananchi ikiwa ni mpango wa kutatua na kushiriki katika mswala ya kijamii.

Sambamba na hilo amewaomba watendaji kushirikana na askari kata hao ambao wapo katika kata mbalimbali hapa nchini ili kukomesha vitendo vya kihalifu katika meneo yao.

Ameeleza kuwa askari kata hao pia wanatakiwa kushirikiana na watendaji hao ikiwa ni Pamoja na kuwapa mafunzo watendaji hao juu ya maswala ya kupambana na uhalifu katika maeneo yao.
Mwisho kamishina Shilogile amewataka watendaji kutumia vyema madawati yansia na watoto kuripoti taarifa za ukatili wa kijinsia ambao amesema katika siku za hivi karibu vimeonekana vitendo vya unyanyasaji kuchuwa nafasi kipindi hiki ambapo amewataka watendaji hao kuto kuwaonea muhali wananchi yeyote atakaye onekana kufanya vitendo vya unyanyasi.

Pia amewaomba watendaji hao kushiriki kikamilifu katika kutoa Ushahidi mahakamani wa viendo vya ukatili wakijinsia na Watoto.