November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Chana: Wazazi tembeleeni vituo vya makumbusho, watoto wawe wazalendo

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Waziri wa utalii hapa nchini Pindi Chana amewataka watanzania hususani wazazi kujijenga Tabia ya kutembelea vituo mbalimbali kama vile makumbusho ya kitaifa ili kuweza kuwahamasisha watoto wawe wazalendo na nchi Yao.

Bado wapo wazazi ambao wanadhana ya kuwa utembeleaji wa vivutio ni muhimu kwa wageni kutoka nje Jambo ambali sio kweli kwani hata watanzania wenyewe wanatakiwa kuwa sehemu ya vivutio hivyo Waziri Chana alisema hayo mapema Jana wakati alipotembelea kituo cha makumbusho ya azimio la Arusha.

Alisema kuwa shuguli za kitalii hata kwa watanzania ni muhimu na Sio kwa wageni pekee na hususani kwa watoto kwani kwa kuwapeleka watoto katika vivutio vya utalii wataweza kuijua Tanzania vyema.

Alibainisha kuwa utalii unachangia kwa kiwango kikubwa Sana pato la taifa na ni muhimu Sana hata watoto nao wakaendelea kujua ili Kuwajengea tamaduni ya kuifadhi na kupenda utalii.

Naye mkurugenzi wa kituo cha azimio la makumbusho Arusha Dkt Gwakisa Kamatula alisema kuwa kituo hicho cha makumbusho ni moja ya vituo ambavyo vinafanya vyema Sana kwa kuwa kina historia kubwa Sana Dkt alisema kuwa hapo awali kituo hicho kilikuwa na changamoto mbalimbali lakini kupitia mradi wa fedha za uviko ambazo zimetolewa na Serikali wameweza kufanya ukarabati mkubwa.

Alisema kuwa wameweza kupokea kiasi cha zaidi ya Milioni 100 ambapo zimeweza kukarabati kituo hicho kwa teknolojia za kisasa ambazo zimefanya makumbusho hiyo kuweza kubaki na historia.

“Tunapenda kualika umma waje waone makumbusho yetu sasa ni ya kisasa Sana na tunashukuru Serikali Sana kwa kuwa fedha ambazo wametupa kwa kweli zimeweza kuwaboresha “aliongeza.

Alihitimisha kwa kuwataka watanzania sasa kutembelea makumbusho hayo ya Azimio la Arusha kwa kuwa hata viingilio vyake ni bei nafuu kwa mtanzania yeyote Yule.