January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mshindi wa NMB MastaBata Kotekote akabidhiwa pikipiki

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mshindi wa shindano la NMB MastaBata KoteKote linaloendeshwa na Benki ya NMB Emmanuel Marumbo kutoka Mkoani Tabora amekabidhiwa rasmi Pikipiki yake leo aina ya Boxer.

Mshindi huyo wa jumla aliyepatikana katika droo ya nane ya shindano hilo iliyofanyika wiki iliyopita Mkoani Tanga, amekabidhiwa zawadi yake na Meneja Masoko NMB Kanda ya Magharibi Trifon Malkiory.

Hafla ya kumkabidhi zawadi hiyo imefanyika leo kwenye Tawi la NMB Mihayo mjini Tabora, ambapo kabla ya kumkabidhi zawadi mshindi Meneja huyo aliendesha droo ya tisa ya shindano hilo kwa wiki hii.Meneja Masoko Trifon amesema kuwa NMB imekuwa ikiendesha shindano hilo ukiwa ni mwaka wa nne tangu limeanza, ambapo linalenga kuhamasisha wateja wake kutumia kadi na Lipa Mkononi (QR).

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya Pikipiki mshindi wa droo ya wiki iliyopita, Emmanuel Marumbo amesema mwanzoni hakuamini kama kweli ameshinda zawadi hiyo licha ya kuwashirikisha wenzake na kuongezea kuwa yeye ni mtu wa kutumia kadi yake ya NMB kwa ajili ya manunuzi ya vitu mbalimbali, huku akibainisha kuwa huwa hatembei na pesa taslimu bali ufanya manunuzi kwa kutumia kadi yake.

Zimesalia siku 10 tu kuelekea grand finale ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu.

Usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote