Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Wakina mama ambao ni Wazazi na walezi wametakiwa kusimamia maadili ya watoto wao ili kuepukana na suala la mmomonyoko wa maadili ambalo limekua changamoto kwa baadhi ya watoto nchini.
Wito huo umetolewa na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania T.I.C Maulana Sheikh Hemedi Jalala Wakati wa maadhimisho ya kusheherekea siku ya mwanamke wa kiislamu duniani ya mtoto wa mtume muhamad s.a w. Fatma a.s ambayo huadhimishwa kama siku ya mwanamke duniani ambapo kiongozi wa mapinduzi wa Iran na kiongozi wa mashia duniani Imam Khomeni alitangaza siku hii kuwa ni siku ya mwanamke duniani
Maadhimisho hayo yalifanyika katika kituo cha utamaduni cha Iran ( Iran Culture ) Jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 13, 2023.
Aidha Sheikh Jalala aliwapongeza wakina mama wote ambao wamehudhuria katika shughuli hiyo lakini pia kwa kupatikana wanawake wanne duniani waliokamilika na walio bora zaidi.
“Nawapa hongera wakina mama wote ambao wamehudhuria katika shughuli hii lakini pia wakina mama wote kwa kukumbuka siku hii kubwa ambayo kiongozi wetu wa kishia aliitangaza siku hii ya kuzaliwa binti mtume muhamad kwamba ni siku ya mwanamke duniani”
“Nawapongeza kwa kupatikana wanawake wanne duniani ambao tunasoma katika maandiko ya kiislamu ambao ni wanawake bora zaidi kuliko wanawake wengine wowote, wanawake waliokamilika” Aliongeza Sheikh Jalala.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake TIC Taifa, Fatma Mwiru alisema katika kuhakikisha watoto wanapata maadili mema kutoka kwa wazazi na walezi wao, wamewapa elimu akina mama wote ambao wamesherehekea siku hiyo ya mwanamke, ili waweze kuyatengeneza yale maadili yote ambayo yameharibika kwakuwa suala la maadili ni suala la mama.
“Duniani kote malezi yameharibika, watoto wamekosa maadili hii ni kutokana na malezi ya mama, hivyo wakina mama ambao tumekutana nao hapa tumewapa ujumbe wa kwamba malezi ambayo yameharibika, maadili ambayo yameharibika wanaoweza kuyatengeneza ni wao kwasababu mama anaweza kila jambo”
“Tumezungumza kuhusu maadili yanavyoweza kubadilika, hii ni kwasababu wakina mama hawana muda wa kutoka na watoto wao, mama akitoka asubuhi kurudi ni usiku” Alisema Mwiru.
Naye Afisa habari wa kamati ya amani mkoa wa Dar es Salaam na mdau wa jeshi la polisi katika dawati la kupinga Ukatili wa Kijinsia mkoa wa kipolisi Ilala na Kinondoni, Dkt. Yatosha Catherine aliwakumbusha Wanawake wote wa kiislamu na wakristo kuwalea watoto katika uangalizi mzuri kwani kwa sasa maadili yamemomonyoka sana kutokana na wazazi kuwa bize sana na kukosa muda wa kukaa na watoto wao.
“Wazazi wakae na watoto wao ili waweze kuzijua tabia zao na kuwaweka katika mazingira mazuri”
“Tunawakumbusha Wanawake wote wa kiislamu na wakristo kuwalea watoto katika uangalizi mzuri kwani kwa sasa maadili yamemomonyoka sana kutokana na wazazi kuwa bize sana na kukosa muda wa kukaa na watoto wao” Aliongeza Dkt. Yatosha
Dkt. Yatosha aliwataka wazazi kuwakagua watoto wao kutokana na suala la ulawiti kuwa mwingi sana na inapogundulika mtoto kafanyiwa kitendo hicho anapaswa kupelekwa kwenye sheria ili sheria ifuate mkondo wake bila kuangalia udini.
Pia Dkt. yatosha alitoa wito kwa akina mama wanaofanyiwa vitendo vya kikatili majumbani, kwamba dawati la jinsia na watoto lipo wazi katika vituo vyote vya polisi wadike na watoe malalamiko yao ili ukatili huo utokomezwe kabisa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa