Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Idadi ya washindi wa kila wiki wa kampeni ya NMB MastaBata KoteKote sasa imefikia 608 baada jana (Ijumaa) kupatikana washindi wa raundi ya 8 ya droo za kila wiki hapa Mtwara ambapo zawadi zenye thamani ya takribani 10m/- zilinyakuliwa.
Kwenye droo hiyo iliyofanyika katika Tawi la NMB Mtwara, wateja 76 wa benki hiyo kiongozi na kinara wa fedha kidijitali nchini walishinda pesa taslimu na pikipiki moja zinazotolewa kila wiki.
Akizungumza kabla ya zoezi la kuwapata washindi hao, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Bi Janeth Shango, alisema wateja 75 watapata 100,000/- kila mmoja na mwingine kunyakua pikipiki aina ya Boxer wiki hii.
Mbali ya droo za kila wiki ambazo mpaka sasa washindi 608 wameshinda zawadi zenye thamani ya kama 84m/- huku thamani ya zawadi za kila mwezi zilizonyakuliwa na washindi 102 ni kiasi cha kama 110m/-, shindano hili pia limehusisha droo mbili za kila mwezi ambapo washindi 98 wamenyakua 1m/- kila mmoja huku wanne wakishinda Boxer kila mmoja wao.
Kwenye droo ya jana, mshindi wa Boxer wa raundi ya saba, Bi Husna Juma Baraka, ambaye ni askari polisi wa Mtwara, alikabidhiwa zawadi yake ya pikipiki.
Zimesalia siku 17 tu kuelekea grand finale ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu.
Usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi