-Aviruhusu vianze mikutano ya hadhara baada ya kusota miaka sita,kumaliza mkwamo mchakato wa Katiba, sheria kufumuliwa imo ya NEC
Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
RAIS Samia Suluhu Hassan, ametangaza uamuzi wa mambo matatualiyofanyiwa kazi baada ya kupokea ripoti ya mapendekezo ya KikosiKazi pamoja na kufanya mikutano na CHADEMA, ambapo ameridhia dai nambamoja kwa kufuta zuio la mikutano ya vyama vya siasa nchi.Rais Samia ametangaza kufuta tangazo hilo Ikulu, jijini Dar es Salaamjana wakati akizungumza na viongozi wa vyama 19 vya siasa vyenyeusajili.
Uamuzi huo wa Rais Samia kufuta tangazo hilo la kuzuia mikutano yavyama vya siasa kunahitimisha zuio lililodumu kwa takriban zaidi yamiaka sita lililokuwa limetangazwa na aliyekuwa Rais wa Serikali yaAwamu ya Tano, Marehemu John Magufuli.
Mbali na kufuta tangazo la zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vyasiasa, Rais Samia ametangaza kuunda Kamati ya Watanzania ambayo kaziyake kubwa itakuwa ni kukwamua mchakato wa Katiba.
Aidha, amesema mchakato wa mabadiliko ya sheria ambazo zilipendekezwakwenye ripoti ya Kikosi Kazi umeanza ikiwemo ya Tume ya Taifa yaUchaguzi (NEC) na kwamba baada ya kumaliza kazi hiyo serikali fursaitatolewa kwa vyama vya siasa na Watanzania kwa ujumla kutoa mawazoyao kuhusu kipi kiondolewe na kipi kibaki.
mikutano ya vyama vya siasa Akianza na mikutano ya vyama vya siasa ambalo alisema lilikuwa dainamba moja, Rais Samia alisema;
“Mikutano ya vyama vya siasa ni haki ya vyama vya siasa. Uwepo wanguhapa leo (jana) ni kuja kutangaza kuwa lile tangazo la kuzuia mikutanoya hadhara sasa linaondoshwa,” alisema Rais Samia huku viongozi wavyama vya siasa wakiimba wimbo wa Tuna Imani na Samia.
“Baada ya kusikia wimbo huo Rais Samia alichomekea; “Kumbe huu wimbo niwa Taifa, nilikuwa ninadhani ni wa kule kwetu (CCM) peke yake.Rais Samia alisisitiza;
“Nina sema mikutano ya hadhara ni haki yavyama vya siasa, lakini ni jukumu lenu kuendesha mikutano ya hadharakwa mujibu wa sheria.Kwa upande wa Serikali wajibu wetu ni kulinda mikutano ya vyama vyasiasa, mnachotakiwa ni kutoa taarifa Polisi na kwa hatua tuliyofikiawajibu wetu ni kuwalinda hadi mnamaliza mikutano yenu salama.Lakini wajibu wenu vyama vya siasa nikufuata sheria na kanunizinavyosema na kama Watanzania tunatoa ruhusa za mikutano ya vyama vyasiasa tukafanye siasa za kujenga na sio kubomoa. Tukafanye siasa zakistaarabu. Sisi ndani ya CCM tunaamini kukosoa na kukosolewa.”
Aonya kuhusu matusiAidha, Rais Samia alivitaka vyama vya siasa kuendesha siasa za kujengamajukwaani na sio kutukanana ili Tanzania iendelee kuwa mfano wakuigwa.
Alisema ni wajibu wa vyama vya siasa kufuata sheria na kanunizinavyosema.
“Kama Watanzania tunatoa ruhusa za mikutano ya vyama vyasiasa tukafanye siasa za kujenga na sio kubomoa.Tukafanye siasa za kistaarabu. Sisi ndani ya CCM tunaamini kukosoa nakukosolewa,” alisema Rais Samia na kuongeza;Mnikinikosoa, mnaniambia nikajikosoe na mkinikosoa nikajikosoa miminaendelea kuwepo.Tusiende kutukanana. Kutukanana sio mila zetu, huo sio utamaduni waWatanzania. Mnaweza mkamtukana Samia Suluhu anaweza kuwa mstamilivu,lakini akatokea chawa wake hasiwezi kustahimili, akaenda akavaana nachawa wako ikawa balaa,” alisema na kuongeza.
“Lakini ukisema waliahidi barabara ya kutoka Kakonko sijui kwenda wapihajajengwa, namuita Mbarawa (Waziri wa Ujenzi) nenda ukafanye hilo,basi na sisi tukiishaijenga tunajua hautakuwa na lingine la kusema.”
“Tukianza kushambuliana kurusha makashifa nchi itakaliwa? Niwaombesana, fursa imetolewa tusiitumie vibaya, irekebishe Serikali, ishauriSerikali.”Alisema pale wanapofanya mazuri wasiache kusema ukweli.
“Najua mtasemaSerikali ina madeni, lakini mueleze imefanya nini. Uongo haujengi,lakini kweli unajenga.
Aingilia kati mkwamo Katiba MpyaKatika hatua nyingine Rais Samia ametangaza kuunda Kamati yaWatanzania itakayoishauri Serikali namna ya kukwamua mchakato waKatiba kwa kuelekeza namna ya kwenda na suala hilo.
“Kwenye suala la Katiba, Tunataka kuanza na Kamati itakayokujakutushauri. Katiba hii ni ya Watanzania. Tunaunda Kamati ya Watanzaniawote ya kutushauri ni namna gani twende . Kwenye Kamati hii kutakuwana wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali.Watakuwepo wanasiasa, wawakilishi wa vyama vya kiraia, wawakilishi wavyombo vya kiraia, wawakilishi wa jumuiya za kimataifa.Tutakuwa na uwakilishi kutoka sehemu zote. Kwa hiyo madai ya Katiba yamuda mrefu sasa yanakwenda kukwamuka na kufanyiwa kazi. Tutakuwa nakamati itakayofanyakazi kwa kupewa hadidu za rejea.Hatutakuwa na Kamati ya lile vuguvugu. Tunataka wakati vuguvugu hilolinaendelea nchi inaendelea na shughuli zake za maendeleo. Tusipojenga vituo vya afya, barabara mtakuja kunipiga kelele, watu hawawezi kulaKatiba…lazima shughuli zingine ziendelee,” alisema Rais Samia.
Mabadiliko ya sheriaAlisema jambo lingine lilikuwa ni la marekebisho sheria kamailivyopendekezwa kwenye ripoti ya kikosi kazi.
Alisema wao kwa upandewa Serikali wameishaanza kufanyia mabadiliko sheria hiyo na kwambahata upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nao wameanza.
Alisema wao wakishamaliza kazi hiyo wanasiasa na wadau watapatiwanafasi ya kutoa maoni yao kwa kuhusu nini wanaona kitoke na kipikibaki.
Alisema hatua iliyofikiwa kwenye mazungumzo na vyama haikuwa rahisi nakuna chama ambacho hakikutaka kushiriki.
Alisema wakati wanazungumzaKinana (Makamu Mwenyekiti wa CCM) na Mbowe (Mwenyekiti CHADEMA)ilikuwa vigumu kuafikiana, lakini sasa hauwezi kujua kama ni wao.
“Leo CHADEMA wamekuja hapa tumewasikiliza na sasa letu moja na hiyondiyo faida ya mazungumzo.Kwenye mazungumzo hakukosekani amani. Hivyo sasa hiyo ndiyo R yakwanza ya maridhiano. Sitaki kusema mazungumzo yamemalizika, badomazungumzo yanaendelea tutazidi kuitana tushauriane, tukubalienetusikubaliane, lakini lazima tukubaliane,” alisema Rais Samia.
Alisema kwa sasa kwa misingi ambayo wanakubaliana watakaa pamoja kamataifa. Alisema ni imani yake wataendelea kukaa pamoja kama walivyokaapamoja kuzungumza mambo yanayohusu nchi yetu.
Alisema” R ya tatu tunafanya mabadiliko ndani ya nchi kwa kuzingatiasheria, mila na desturu zetu na matamko ya kimataifa. Sio matamko yakimataifa yanatoka huko tunayabeba kama yalivyo, bali kwa kuzingatiamila na desturi ili kujenga taifa la Watanzania wenye kuamini nchiyao,”alisema Rais Samia na kuongeza;
“Huko ndiko mwenyezi Mungu amenielekeza tuelekee na nina imaniwenzangu mtaniunga mkono tuelekee huko. Dhana hii imepata baraka yachama changu na ninyi mtaniunga mkono tuelekee huko.Tunataka Tanzania ikisimama dunia nzima inajua kuna nchi imewika.Tanzania imewika, Tanzania imesema.Serikali inataka kutenda haki kwa watu wote hatuwzi kutenda haki kwakuiga hata kama zinapingana na mila na desturi. Lengo ni kujenga Taifalenye ushirikiano, upendo na mshikamano kwa ajili ya nchi yetu.”
Alisema ili kufika huko, kila mmoja wetu ana wajibu wa kufanya namsingi wa yote ni amani ndani ya nchi yetu.
Mapendekezo ya kikosi kazi kubwa lililoletwa ilikuwa ni mikutano yahadhara na mabadiliko ya sheria na juzi alikuwa na NEC nao wapo njianiya kubadilisha sheria ya uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa.
Alisema wakati zinafanyiwa kazi lazima wadau wote watoe mawazo yaohivyo baada ya kumaliza Serikalini watawaitwa ili waone tunakwendawapi, lengo ni ili haki za vyama vya siasa zinaonekana.
“Tunauanza mwaka tukiwa tumetoa ruhusa kwa mikutano ya vyama vya siasana pia mabadiliko ya sheria mbalimbali yanaendelea na tunakwendakukwamua suala la Katiba,” alisema.
Alisema kamba tumeifungua na ndivyo inavyotakiwa na sio kuruhusumikutano vya vyama vya siasa mwende mkafanye fujo.Alisisitiza tutakwenda kwa katiba, sheria na mila ya desturi na siokwenda kuharibu Taifa.
“Dhamira yangu ni kuongoza Taifa lenyemaendeleo makubwa.Nakupa ndiyo, tunakopa kwa maendeleo ya Taifa na mimi nataka nimalizemitano yangu hii hadi 2025 nikiwa nimeifanyia kitu Tanzania,” alisemaRais Samia.
Alipokabidhiwa nchiAwali Rais Samia aliwashukuru viongozi wa vyama vya siasa kwakuitikioa wito huo ili kwenda kuona nini wanataka kuzungumza kwamustakabali wa nchi yetu.
Alisema ameitisha kikao hicho kuna mambo ambayo walizungumzawalikubaliana na anataka kuyatolea maamuzi.
Alisema wakati anakabidhiwa kuongoza nchi busara zilimtuma jinsialivyopokea hilo, aliona kuna haja ya kufanya taifa kuwa kitukimoja,wote wazungumze lugha moja.
Alisema ili Taifa liwe moja, lazima wawe na maridhiano na kwenyemaridhiano sisi ya vyama vya siasa tu, kwani vinawakilisha watu.
“Ni kasema kwanza tuwe na mazungumzo na vyama vya siasa. kwa hiyotukakubaliana tuzungumze ndani ya vyama tukaunda kikosi kazi kikaja namaamuzi,” alisema Rais Samia.
Jaji Francis MutungiAwali Msajili wa Vyama vya Siasa,Jaji Francis Mutungi alisema kitendocha viongozi hao kuhudhuria mkutano huo bila kukosa ni mwanzo mpya nashauku ya kumsikiliza Rais Samia.
Alisema umma wa Watanzania na mataifa ya nje wanasubiri kuonautawaambia nini.
Alisema watajitaidi kufanyakazi zao kwa weledi.Alisema mapungufu aliyoyaona mwaka uliopita sio watakaoenda nayo sasahivi.
“Pale utakapoona kuna haja na marekebisho ya sheria basi yafanyikemapema,” alisema.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa