Na Mwandishi Wetu, TimesMajiraOnlin, Dodoma
RAIS Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kuongoza chama kikongwe barani Afrika kwa kuchaguliwa kwa kura endapo Mkutano Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utamchangua kuwa mwenyekitti wa chama hicho kwa miaka mitano ijayo.
Dkt. Samia amekuwa mwenyekiti wa CCM kwa kurithi nafasi hiyo kufuatia kifo cha Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM.
Jana Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilipitisha jina Rais Dkt.Samia kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mwaka 2022 hadi 2027.
Endapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utamchangua Dkt. Samia kuwa mwenyekiti wa CCM, atakuwa ameandika rekodi nyingine kwa mwanamke wa kwanza kuongoza chama hicho kikongwe barani Afrika baada ya kuchaguliwa kwa kura.
Wenyeviti wa CCM waliotanguliwa kuongoza chama hicho ni Pamoja na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Rais Msataafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwenyi na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa.
Wengine ni Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli. Leo, matokeo ya kura za wajumbe wa mkutano Mkuu ndiyo yanasubiriwa kwa hamu kuamua rekodi mpya ya Dkt. Samia iwapo atachaguliwa kushika wadhifa huo.
More Stories
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi
Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha