December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbasha awaasa wazazi Holly Land kuwekeza kwenye elimu

Na Esther Macha,Timesmajira, Online, Chunya

MLEZI wa waimbaji wa nyimbo za Injili nchini na mchimbaji wa madini amewataka wazazi na walezi kuwekeza kwenye elimu kwa ajili ya watoto na kuwa mtoto anapokuwa na elimu mzazi anakuwa amemfungulia njia ya maisha yake .

Amesema kuwa hakuna maisha ya mkato ya kuwasaidia watoto bila ya kuwa na elimu katika maisha yao.

Mbasha amesema hayo leo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya nne ya shule awali na msingi mchepuo wa kiingereza Holly Land inayomilikiwa na Lawena Nsonda (Baba mzazi)iliyopo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongolosi iliyopo wilayani Chunya.

“Mtoto anapokuwa na elimu ndivyo anaweza kusonga mbele katika maisha yake ya baadaye,hakuna maisha ya mkato ambayo sisi wazazi tunaweza kuwapa watoto wetu zaidi ya elimu mtoto anapokuwa na elimu unazidi kumfungua katika maisha yake ya baadaye kwani mtoto anapokuwa na elimu na kumaliza elimu yake yote anaweza kufanya biashara yeyote nje ya nchi “amesema Mbasha.

Hata hivyo Mlezi huyo wa waimbaji nchini amesema sema kuwa mpaka sasa Rais Samia Suluhu Hassan amefungua masoko ya dhahabu mengi nje ya nchi masoko mengi ya dhahabu hivyo mtoto anapokuwa amesoma anaweza Uingereza , Dubai na nchi zingine kwasababu anakuwa na uwezo mpana wa kujua vitu pamoja kufahamu lugha ya Kiingereza.Katika mahafali hayo Mbasaha alichangia zaidi ya shilingi mil.2.na kuwataka` wazazi kuzidizi kuwekeza kwenye elimu zaidi .

Mkuu wa shule ya ya Holly Land , Yona Mwakalinga amesema kuwa shule hiyo ina changamoto mbali mbali ambazo zinaikabili shule ikiwemo uhaba wa majengoNaye msanii na mchekeshaji maarufu nchini Oscar Petro(Oscar Nyerere) amesema uwekezaji uliofanywa na Lawena Nsonda ni sehemu ya sadaka kwenye jamii hivyo anapaswa kuungwa mkono na`wadau katika suala nzima la kuinua elimu katika wilaya ya Chunya ambayo siku za nyuma ilikuwa nyuma katika suala la elimu .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule Lawena Nsonda amesema ushirikiano baina yake na watumishi ndiyo chanzo cha mafanikio cha shule hiyo .

Amesema ushirikiano huo umekuwa ukisaidia sana katika elimu ,walimu wanajituma sana katika kazi hiyo ya kufundisha watoto ,walimu wote wapo kitu kimoja kuanzia mkurugenzi mpaka wapishi.

“Walimu shuleni hapa ni cheni moja kwani ukifika shuleni hapa huwezi kujua mwalimu ni yupi na mkurugenzi ni yupi wote ni cheni moja tunapovuta kamba moja lazima mafanikio lazima yawepo kwa kiasi kikubwa”amesema Mkurugenzi huyo.

Shule ya Holly Land ilianza mwaka 2019 ikiwa na watoto wawili ambapo mpaka sasa ina watoto zaidi ya mia tatu hamsini huku ikiendelea kufanya vema Kiwilaya,Kimkoa na Kitaifa ambapo mwaka jana iliongoza mtihani wa darasa la nne kitaifa na kushika nafasi ya kwanza.

Shule ya awali na msingi mchepuo wa kiingereza Holly Land Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya inayomilikiwa na Lawena Nsonda(Baba Mzazi) imefanya mahafali ya nne ya kuhitimu watoto wa darasa la awali mgeni rasmi akiwa ni Emmanuel Mbasha mchimbaji wa madini na mlezi wa waimbaji wa nyimbo za injili nchini.