NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspar Mmuya Oktoba 25, 2022 ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji inayohusisha Makatibu Wakuu Kwaajili ya Maandalizi ya Uzinduzi Wa Matokeo Ya Kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi Utakaofanyika Oktoba 31,2022 Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Dodoma.
“Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kikao hicho”
Ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
“Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu Bi. Ruth Minja akitoa taarifa ya mwongozo wa uzinduzi huo utakavyofanyika wakati wa kikao hicho”
“Baadhi ya Makatibu wa Wakuu wakifuatilia hoja za kikao hicho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael, katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban na Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba, na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi”
“Mratibu wa Sensa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Adela Mpina akitolea ufafanuzi baadhi ya taarifa zilizowasilishwa za maandalizi ya Uzinduzi huo”
More Stories
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Baraza la Taifa la Ujenzi waingia makubaliano ya mashirikiano sekta ya ujenzi
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu ujerumani
Taarifa za maendeleo ziwafikie wananchi kwa usahihi