January 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia: Mmenifurahisha sana Watoto wangu

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Samia Suluhu Hassan, amefurahishwa na matokeo walioyoapata timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Girls’ katika michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake U-17 inayoendelea nchini India dhidi ya Canada

Katika michuano hiyo, Serengeti Girls, imefuzu kuingia robo fainali za Kombe la Dunia baada ya kutoka sare ya goli 1-1 ndhidi ya Canada, katika mchezo wa mwisho wa kundi D kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kwa umri huo uliochezwa kwenye uwanja wa la DY Patil Navi – Mumbai nchini India.

Akiwapa pongezi hizo Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia ameonesha kufurahishwa na vijana hao kutokana na mafanikio waliyopata kwenye michuano hiyo.

”Mmenifurahisha sana Watoto wangu Serengetigirls kwa kuandika historia ya kufuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 nchini India.

“Mmefanya jambo kubwa kwa nchi yetu Tanzania na nawatakia kheri katika hatua ya robo fainali,”- ameaandika Rais Samia Suluhu Hassan.