January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Parimatch Tanzania yaingia makubaliano ya mkataba wa udhamini wa klabu ya Mbeya City

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Kampuni ya Parimatch Tanzania imeingia rasmi makubaliano ya mkataba wa udhamini wa klabu ya jiji la Mbeya ‘Mbeya City’ ambayo inashiriki michuano ya ligi kuu Tanzania Bara katika msimu huu wa 2022/2023.

Katika makubaliano hayo, Parimatch itatoa vifaa kwa klabu pamoja na ukarabati mdogo wa uwanja wa sokoine hasa katika eneo la kukaa la benchi la ufundi kwa awamu ili kuufanya uwanja kuendelea kuwa na sifa ya kuchezewa michezo ya ligi kuu

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Agosti 9, 2022 Afisa Habari wa Parimatch Tanzania Ismael Mohamed alisema makubaliano hayo yamekuja baada ya klabu hiyo kuwa kubwa kwa Tanzania hususani idadi ya mashabiki na ushawishi katika soka .

Ismael alisema mbali na kuendelea kuunga mkono mbeya city ili mashabiki wa soka waendelee kupata burudani stahiki, wataendelea pia kuunga mkono vilabu vingine;

“Tunaendelea na michakato mbalimbali ya kuunga mkono vilabu vingine kutoka ligi kuu, ligi daraja la kwanza na hata vilabu chipukizi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za TFF na bodi ya ligi kuhakikisha ligi za Tanzania zinakuwa na tunaenda kimataifa “

Mbali na hayo Ismael alisema jukumu lao kubwa ni kuhakikisha michezo inakua kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya kimataifa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu Mbeya City FC, Emmanuel Kimbe aliwaahidi Parimatch ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kile wanachotakiwa kukifanya Lakini pia aliushukuru uongozi wa Parimatch kwa kufanya kazi nao kwa msimu huu mwingine wa 2022/23.

“Kwetu mmekuja sehemu sahihi na hamtojutia kuwa na sisi hivyo tutawapa Kile mnachohitaji,”

Pia Kimbe aliwashukuru Parimatch kwa kuwarekebishia uwanja wa sokoine ambao utasaidia Watu wote wanaotumia uwanja huo ambao utaongeza Uchumi wa jiji la Mbeya.