Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Ni wiki kadhaa sasa tangu Tigo Zantel itangaze rasmi kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya mbio maarufu za Zanzibar International Marathon zinazotarajiwa kufanyika Tarehe 7 Agost 2022 visiwani Zanzibar huku zikiwa na lengo la kutangaza utalii nchini.
Akizungumza Leo Agosti 5, zikiwa zimebakia siku mbili kuelekea mbio hizo Mkurugenzi wa Tigo Zantel Kanda ya Zanzibar Ndg. Emmanuel Joshua amewasihi kuendelea kujisajili kwa ajili ya mbio hizo zenye lengo la kutangaza utalii wa nchi.
” Kama mnavyojua Tigo Zantel tuna uzoefu mkubwa katika kudhamini mbio nyingi za kimataifa kwahyo tunatoa wito kwa watu kuendelea kujisajili kwa wingi ili kushiriki mbio hizi , kwa kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tunawahakikishia washiriki wote usalama wa hali ya juu , kumbuka unaweza kununua tiketi yako kupitia lipa kwa simu namba 5121222 Au Piga*150*01# au tumia Tigo Pesa app kwa kuscan chap kirahisi.
Na Namba za kukimbia zimeanza kutolewa tangu tar 1 Agosti katika vituo mbalimbali kama Catalunya-in-Zanzibar, Michenzani Mall Zanzibar, Just fit kijitonyama Dar Es Salaam pia waweza kutembelea vituo ivyo kwa ajili ya kujipatia tiketi yako , Karibu tukimbie pamoja kuboresha afya Zetu ” Alimalizia.
Nao kwa wakati tofautitofauti wakazi wa Zanzibar wametoa hamasa kwa watu kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizi za kimataifa huku wakisisitiza kuwa Zanzibar ni Salama atakae na aje .
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania