April 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tazama VETA ilivyobuni mashine ya kukaushia nguo za ndani

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

WATANZANIA wameaswa kuzikubali na kununua teknlojia zinazobuniwa na wazawa ili kuwahamasisha wabunifu kuendelea kubuni bidhaa mbalimbali zinazotatua changamoto katika jamii.

Akizungumza katika viwanja vya John Mwakangale kwenye maonyesho ya Wakulima na wafugaji Nane Nane Mwalimu na Mbunifu kutoka Chuo cha VETA Dar es Salaam Mwalimu  Emmanuel Bukuku ,amesema kumekuwa na desturi ya watanzania kuamini bidhaa zinazotoka nje kuliko bidhaa zinazolishwa hapa nchini.

Mwalimu huyo ambaye amebuni kifaa cha kukaushia nguo za ndani kinachoitwa Dhydrator mashine kwa ajili ya kupunguza au kutokomeza kabisa  magonjwa  Fangasi ya ngozi na U.T.I amesema,Mamlaka ya Elimu nchini (VETA) kupitia vyuo vyake vilivyopo hapa nchini,vimeuwa vikifanya bunifu nyingi pamoja na Urinary Tract Infection, U.T.I.

Mwalimu Bukuku kutoka Chuo cha VETA Dar Es Salaam akiwa katika maonyesho ya wakulima na Wafugaji Nane Nane Jijini Mbeya akionyesha mashine ya kukaushia nguo za ndani inavyofanya kazi .Mashine hiyo inafanya kazi hiyo lakini pia inatumika kama ‘Dressing table’

Mwalimu Bukuku amesema kuwa amebuni mashine hiyo baada ya kuona kuna changamoto ya uanikaji wa nguo za ndani ambayo inaweza kusababisha magonjwa mbalimbali kwa wananchi kwa kuvaa nguo hizo kabla hazijakauka kutoka na kuanika kwa kuzificha ficha.

“Baada ya kuona changamoto ya uanikaji wa nguo za ndani nilikaa chini na kubuni mashine inayotumia umeme kidogo ambayo itaondoa  changamoto hiyo ya kukausha nguo hizo kwa muda mfupi na kumwezesha mtumia kuivaa huku akijihakikishia usalama.”amesema Mwalimu Bukuku

Amesema kuwa nguo za ndani mara nyingi zikifuliwa huwa zinaanikwa ndani hali inayowasababishia watumiaji kupata magonjwa kutokana na kukuza wadudu ambao wanasababisha magonjwa kama Fangasi.

Amesema,katika jamii ipo changamoto ya  kupata magonjwa kama vile Fangasi ya ngozi na U.T.I  kwa watu wazima na watoto hivyo kifaa hicho kitasaidia kupunguza magonjwa hayo au kuyatokomeza kabisha.

Mwalimu Bukuku amefafanua kuwa mashine hiyo ametengeneza kwa muda wa wiki tatu na kuifanyia majaribio ambapo ilionesha ipo vizuri na inauzwa kwa shilingi 350,000 huku akisema mashine ipo kama dressing table ambapo mtumiaji atanufanika na vitu viwili atatumia kukuangalia kupitia kioo na chini kukaushia nguo za ndani.

” Kwa upande wa afya  hii ni teknolojia nzuri na jamii bado haijajua hii mashine  kwa ubunifu huu tunaweza kuwakomboa watoto wengi wanaokumbana na magonjwa ya U.T.I na Fangasi, pamoja na wanawake hii inaweza kuwa mkombozi kwao,”amesema na kuongeza kuwa

“Katika maonesho ya mwaka huu ya Nane nane VETA tumeweza kuja na teknolojia mbalimbali ikiwemo mashine ya kukaushia nguo za ndani,”