November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauri ya Meru yapata elimu ya kukabiliana na maafa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado amesema elimu ya usimamizi wa Maafa itaendelea kutolewa kwa wananchi kwa maeneo yanaoathirika kwa matukio ya tofauti tofauti ya maafa.

“Tunatoa elimu kwa wananchi ili kujenga uelewa wanamna ya kukabiliana na maafa, kwa kueleza dhana ya maafa, kueleza maana ya majanga ikiwa pamoja na kuangalia mzingo wa maafa kwa ujumla”

Hayo yamesemwa na Luteni Kanali Selestine Masalamado Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) katika kikao cha mafunzo ya Udhibiti wa Maafa kwa jamii yaliyofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuhusisha wananchi wa kata ya Mbuguni na Shambaray Bruka.

“Washiriki wameelewa mfumo mzima wa Kudhibiti Maafa kwa kuanzia ngazi ya taifa hadi kufikia ngazi ya Kijiji, alisema Luteni Kanali”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameshukuru Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa kufanya mafunzo hayo Halmashauri ya wilaya ya Meru.

“Tunashukuru kwa kutuongezea wataalamu wa maafa kupitia mafunzo yaliyoyotolewa ili kutusaidia namna ya kukabiliana na Maafa.”

Mwl. Makwinya amefanunua kata ya Shambaray Bruka na Mbuguni yamekuwa yakiathirika na mafuriko na ukame,

Ametoa wito kwa washiriki kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza maarifa kwa kusaidia maeneo mengine yanayoyoathirika na maafa.

Naye Mshiriki Fanael Kaaya Mshiriki kutoka kata ya Mbuguni amesema mafunzo ya kukabiliana na maafa waliyopata imesaidia kuchukua tahadhari ya kujikinga na maafa kabla hajatokea ikiwemo kutengeneza matuta ya kuzuia maji kwenye maeneo yanayoathirika na mafuriko na pamoja kufukua mifereji iliyoziba pamoja na mito ili mafuriko ya maji yanapokuja yaweze kupita.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado akizungumza na washiriki wa mafunzo ya elimu ya kukabiliana na Maafa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akizungumza na washiriki wa mafunzo ya elimu ya kukabiliana na maafa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado akiwa na washiriki walio katika makundi wakati wa mafunzo ya elimu ya kukabiliana na Maafa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Dkt. Baltazari Leba Mratibu wa Idara ya menejimenti ya maafa Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akiwa na washiriki wakati mafunzo ya elimu ya kukabiliana na maafa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.