November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu CCM ajiuzuru, Wananchi wamkalia kooni Mwenyekiti Chanika

Na David John, Timesmajira online

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Shina namba 11 lilipo Mtaa wa Ngobedi kata ya Zingiziwa Chanika wilayani Ilala, Dorah Musiba na wajumbe wawili wa kamati ya shina hilo wamejiuzuru nafasi zao kwa kile walichodai kushindwa kuelewana na Mwenyekiti wa shina hilo, Salma Waziri Msangi.

Katibu huyo amesema kuwa tangu walivyochaguliwa katika nafasi hizo wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ya kutokuelewana na kiongozi wao mkuu ambaye ni mwenyekiti, hivyo kwa kunusuru chama chao wameona wakae pembeni, wakibaki kuwa wanachama wakawaida.

Ametangaza uamuzi huo katika mkutano maalumu wa wanachama
na wananchi wa shina hilo na 11 uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM tawi la Ngobedi, Sefu Machucha na katibu wake, Anaclet Mizambwa.

Dorah amesema analazimika kujiudhuru kwa sababu anashindwa kufanya kazi na mwenyekiti huyo kwa madai kuwa mwenyekiti hataki kushirikiana na katibu wake.

”Ndugu zangu wanachama wezangu nimesimama hapa nikiwa
na mapenzi makubwa na Chama changu, lakini kuazia sasa natangaza kujiudhuru nafasi yangu ya ukatibu kwa sababu nimeshindwa kufanya kazi na mwenyekiti, amekuwa akisema hawezi kufanya kazi na mimi kutokana na ujane wangu lakini pia amekuwa akisema mimi ni mjane, hivyo hawezi kufanya kazi na mtu anayejifanya anajua,”alisema

Dorah na kuongeza; ‘Mwenyekiti huyu amekuwa akisema hamtambui licha ya kuchaguliwa na wananchi kwa kura 57 za ndio nakwamba hausiki kwa lolote kwenye hilo shina na hawezi kufanya kazi na mjane.kwa hiyo mimi naamua kujiudhuru mbele yenu viongozi,”alisisitiza Dorah

kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya shina hilo. Ally Omari na Maria Laswai nao wamejiudhuru kwa madai kuwa tayari hawawezi kufanya kazi mahala ambapo pana mpasuko .

”Hapa panashida kubwa kama mwenyekiti na katibu hawaelewani
kuna uongozi tena ? ” Walihoji wajumbe je tutafanyaje kazi, huu ni mpasuko ndani ya chama chetu, hata ninyi waandishi mmeona tena mambo haya yanatokea mbele ya viongozi wetu wa tawi mwenyekiti yupo hapa na katibu wake lakini pia Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa Mohamedi Kilungi naye yupo. tumeshandaa barua ya kujiudhulu.”walisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa tawi la Ngobeni la CCM ambaye
ndio bosi wao, aliposimama kutoa ufafanuzi wa utaratibu uliopo ndani ya chama chao, hakueleweka kutokana na wana CCM kupaza sauti za kumkataa mwenyekiti wao.

Naye katibu wa tawi hilo, Anaclet Mizambwa akizungumzia utaratibu wa chama alisema kuwa katibu pamoja na wajumbe wa kamati waliojuhudhuru wanapaswa kuandika barua na maelezo
ya kujiudhuru kwao kwa uongozi wa CCM ngazi ya tawi ili kuweza
kuyafanyia kazi ila wao kama viongozi kwa kile ambacho walikuwa wanataka wananchi kwa maana ya kuchukua hatua dhidi ya kiongozi anayelalamikiwa hawawezi kumuondoa pasipo utaratibu
ukizingatiwa.

Mwenyekiti wa shina anayelalamikiwa, Salma Msangi alipofuatwa ili kujibu tuhumu za wananchi wake na wanachama, aligoma kuzungumza na vyombo vya habari kwa madai kuwa yeye hawezi kusema chochote.

Awali katika kikao hicho Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ngobedi Mohamed Kilungi kutokana na mvutano uliojitokeza alisikika akisema shina hilo kuna changamoto kubwa na ikiwezekana uchaguzi urudiwe upya kwa sababu hali ilivyo hawawezi kufanya kazi kiufanisi.