Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
MBUNGE wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amempongeza Diwani wa Segerea Robert Manangwa katika ziara yake Leo Segerea Wilayani Ilala.
Mbunge Bonah alisema anampongeza Diwani Robart Kwa kuweka vipaumbele vyake katika kata ya SEGEREA katika juhudi za kutatua kero na kuisaidia Serikali.
“Nakupongeza MH,Robart Kwa kusaidia Wananchi wangu wa Segerea vipaumbele vyako sita vya Maendeleo katika kata ya SEGEREA umeviweka wazi Ili utatue KERO hizo za Wananchi wetu wapate Maendeleo” alisema Bonah .
Mbunge Bonah aliwataka wakazi waSegeea kutangaza kazi za MH Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani .
Aliwapongeza viongozi wapya wa chama Cha Mapinduzi ngazi za matawi wajipange Kwa ajili ya kushika Dola 2025 pia wasimamie miradi vizuri ya Serikali ambayo imeibuliwa .
Alisema pesa za serikali awali zilipokelewa shilingi milioni 500 fedha za Jimbo ambazo zimejenga kipande Cha Barabara ya Kipawa ,fedha zote zitakazotolewa na SERIKALI lazima tuziwekee bajeti katika Lami .
Akizungumzia mradi wa Barabara za Kisasa UDMP zilizopewa kipaumbele Segerea alisema ujenzi wa Barabara hizo unatarajia kuanza hivi karibuni taratibu zake zimekamilika Serikali imeshapitisha.
Diwani wa Kata ya Segerea Robart Manangwa alisema mikakati yake Kata ya Segerea ya Maendeleo kuijenga Segerea ya Kisasa vipaumbele sita anatarajia kuvitekeleza katika utekelezaji wa Ilani
Diwani Robart alitaja vipaumbele hivyo ambavyo ni Barabara ,kituo Cha Afya,Soko standi ya Daladala ,Kituo cha Polisi .
Alisema akizungumzia ujenzi wa soko la Segerea fedha zimetoka shilingi milioni 75 tenda ya ujenzi imeshatangazwa tayari ujenzi unaanza .
Alisema katika vipaumbele vyake vya Barabara NANE segerea zikingine zimeingizwa katika mradi wa Barabara za Kisasa DMDP Barabara tatu ambazo ni Segerea Oil Com Stakishari,Changombe Mbuyuni ,na Barabara Tano za TARURA .
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi