November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NMB yatoa bati na madawati ya sh. milioni 11 Lushoto

Na Yusuph Mussa, TimesMajira Online, Lushoto

BENKI ya NMB imetoa bati 200 zenye thamani ya sh. milioni saba kwa Zahanati ya Kwemakame, na madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) Shule ya Msingi Mbula B, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Msaada huo ulikabidhiwa Julai 12, 2022 kwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro, na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper kwenye hafla fupi iliyofanyika Shule ya Msingi Mbula B.

Akikabidhi msaada huo, Prosper alisema wanathamini jitihada za Serikali kuweza kuimarisha huduma za jamii ikiwemo elimu, afya na maji. Hivyo, wao kama sehemu ya jamii, nao wana mchango mkubwa kuona wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu na afya.

“Pamoja na makubwa yanayofanywa na Serikali, sisi kama wadau tunao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleio kwa kusaidia jamii zetu, kwani jamii hizi ndiyo zimeifanya Benki ya NMB kuwa hapa ilipo, na kubwa kuliko benki yeyote hapa nchini.

“Tulipopata maombi haya ya kuchangia katika maendeleo ya elimu kwa Wilaya ya Lushoto, tulifarijika na kuamua mara moja kuja kushirikiana nanyi ili kuwa chachu ya maendeleo ya Sekta ya Afya na Elimu kwa jamii yetu hasa katika Zahanati ya Kwemakame na kwa Shule ya Msingi Mbula B” alisema Prosper.

Prosper alisema kwa miaka mingi sasa, Benki ya NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu na afya ikiwemo kutoa vitanda, magodoro na vifaa tiba, huku wakisaidia majanga yanayoipata nchi, na hiyo ni kutambua kuwa, kupitia jamii ndipo wateja wao wengi wanapotoka, hivyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni wao.

Mkuu wa Wilaya, Lazaro alisema Benki ya NMB ni ya kuigwa nchini, kwani imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kuimarisha miundombinu ya elimu na afya ili kuona watoto wanapata elimu sehrmu bora, na wananchi wanapata huduma za afya.

Lazaro alisema, hata huduma zake za kifedha katika kutoa mikopo ni nzuri, kwani makundi mengi ya wanawake na vijana ikiwemo bodaboda, pia wanapata mikopo kwa masharti nafuu, na kuweza kuwa wajasiriamali na kuinua kipato cha kila mmoja wao.

Naye William Pius, Mtendaji wa Kijiji cha Kwemakame, alishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo, kwani utasaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati yao, huku Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbula B, Reuben Masenga, akisema madawati waliyopata ni ukombozi kwa watoto wake kuona wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Ikupa Mwasyoge alisema pamoja na Serikali kuimarisha miundombinu ya shule, zahanati na vituo vya afya, bado wanawashukuru wadau mbalimbali kama Benki ya NMB kwa kuweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye elimu na afya.

“Msaada huu waliotupa wa mabati 200 kwa ajili ya Zahanati ya Kwenakame, na madawati 50 kwenye Shule ya Msingi Mbula B, ni sehemu ya msaada wanaoendelea kuutoa Benki ya NMB. Kwani, pamoja na Serikali kufanya maboresho makubwa kwenye huduma za jamii kama elimu, afya na maji, bado wadau wetu kama Benki ya NMB wameendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha miundombinu” alisema Mwasyoge.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalisti Lazaro (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya NMB, viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbula B. Ni baada ya hafla ya NMB kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) kwa shule hiyo. (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalisti Lazaro (kulia) akizungumza kwenye hafla fupi ya NMB kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) kwa Shule ya Msingi Mbula B, na bati 200 zenye thamani ya sh. milioni saba kwa Zahanati ya Kwemakame . Hafla hiyo ilifanyika Shule ya Msingi Mbule B. Wengine kwenye picha ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (katikati), na Meneja Uhusiano wa NMB Kanda ya Kaskazini Christabela Hiza. (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalisti Lazaro (wa nne kulia) akipokea bati kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (wa nne kushoto). Ni baada ya hafla ya NMB kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) kwa Shule ya Msingi Mbula B, na bati 200 zenye thamani ya sh. milioni saba Zahanati ya Kwemakame kwenye hafla fupi iliyofanyika Shule ya Msingi Mbula B . (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Kalisti Lazaro (wa pili kushoto) akipokea dawati kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (wa tatu kushoto). Ni baada ya hafla ya NMB kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) kwa Shule ya Msingi Mbula B, na bati 200 zenye thamani ya sh. milioni saba Zahanati ya Kwemakame kwenye hafla fupi iliyofanyika Shule ya Msingi Mbula B . Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Ikupa Mwasyoge. (Picha na Yusuph Mussa).
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper (wa pili kushoto) akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi bati 200 zenye thamani ya sh. milioni saba kwa ajili ya Zahanati ya Kwemakame na madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) kwa Shule ya Msingi Mbula B. Hafla hiyo ilifanyika Shule ya Msingi Mbula B. Wengine kwenye picha ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mathew Mbaruku (kulia), na Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Christabela Hiza (kushoto). Picha na Yusuph Mussa).
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbula B walikuwepo. Ni kwenye hafla fupi ya NMB kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) kwa Shule ya Msingi Mbula B, na bati 200 zenye thamani ya sh. milioni saba Zahanati ya Kwemakame kwenye hafla fupi iliyofanyika Shule ya Msingi Mbula B . (Picha na Yusuph Mussa).
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbula B walikuwepo. Ni kwenye hafla fupi ya NMB kukabidhi madawati 50 yenye thamani ya sh. milioni nne (4) kwa Shule ya Msingi Mbula B, na bati 200 zenye thamani ya sh. milioni saba Zahanati ya Kwemakame kwenye hafla fupi iliyofanyika Shule ya Msingi Mbula B . (Picha na Yusuph Mussa).