November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama. (Picha na Mtandao).

Rais Obama ayapa tano maandamano mfululizo Marekani kupinga kifo cha Mmarekani mwenye asili ya Afrika

Na Mwandishi Wetu

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amesema kuwa, anaamini Marekani itakuwa bora kwa kuwa vijana mstari wa mbele kushinikiza mabadiliko kupitia maandamano yanayoendelea kushuhudiwa kila kona ya nchi hiyo.

Obama kupitia hotuba yake ya kwanza tangu raia wa Marekani mwenye asili ya Kiafrika, George Floyd kuuawa katika mazingira yaliyoibua utata na mjadala mkubwa wa kitaifa amesema, kuna tofauti kubwa kati ya sasa na miaka ya 60 iliyopita.

Ni miaka ambapo harakati za kutetea haki za wachache katika jamii, hazikutekelezwa na watu wa tabaka mbalimbali kama ilivyo sasa.

“Nimesikia baadhi ya watu wakisema msukumo huu unaoendelea sasa unawakumbusha maiaka ya sitini. Lakini ukiangalia sasa, kuna tofauti.Ni wakati wa kila mmoja kutembea anakotaka bila kuwa na wasiwasi wa kushambuliwa,”amenukuliwa Obama wakati wa mkutano kwa njia ya mtandao uliofadhiliwa na Shirika la Wakfu wa Obama.