Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, DSM
Wizara ya Maliasili na Utalii imekabidhiwa magari kumi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili wa wanyamapori.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa magari hayo, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii , Prof. Eliamani Sedoyeka amesema Magari hayo yanakwenda kwenye kaya 10 tofauti tofauti kwa lengo la kuhakikisha kuwa rasilimali za wanyamapori zinalindwa kikamilifu.
“Nchi yetu ipo katika mapambano makali dhidi ya ujangili na sisi kama wizara ya maliasili tuna jukumu la kuhakikisha rasilimali zetu zinaendelea kutumikakwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo”
Amesema Prof. Sedoyeka Amesisitiza kuwa katika jitihada za kupambana na ujangili, Wizara imeendelea kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi ikiwemo UNDP,
“UNDP imetusaidia katika kuijengea uwezo timu yetu pamoja na kutuongezea vitendea kazi ambapo leo hii wametukabidhi magari 10 kwa ajili ya mapambano hayo”
Kutokana na jitihada hizo, Prof. Sedoyeka amesema odadi ya wanyama wakubwa kama vile tembo ba faru waliokuwa wakipungua kutokana na tatizo la ujangili wameanza kuongezeka kwa kasi.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Christine Musisi amesema kumekuwa na ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kipindi cha muda mrefu na hivyo wamekuwa wakivutiwa na juhudi zinazofanywa na Wizara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili wa wanyamapori
” Tumeendelea kushirikiana na Wizara kwa kuwapatia vitendea kazi, kuwajengea uwezo watumishi na kupitia jitihada hizo idadi ya wanyama kama vile tembo imeongezeka maradufu,”alisema Mwakilishi wa UNDP
Musisi Mwakilishi huyo wa UNDP amesisitiza kuwa UNDP itaendelea kuwa mdau mkubwa wa uhifadhi kwa kuhakikisha kuwa wanyamapori wa Tanzania wanaendelea kuwa salama kwa ajili ya manufaa makubwa ta jamii na uchumi wa nchi.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili