Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mbio za baiskeli zijulikanazo kwa jina la ‘Africa Classic ‘ zinazoratibiwa na shirika la Amref Netherlands kwa kushirikiana na Amref Africa zimefunguliwa rasmi Juni 12, 2022 Mkoani Kilimanjaro.
Katika mbio hizo Raia zaidi ya 40 wameanza mbio hizo kwa kuzunguka mlima Kilimanjaro kilometa 400 kwa siku sita kuanzia juni 12 hadi 18 kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili itafanyika Juni 19 hadi 25 ambapo waendesha baiskeli 67 watashirika mbio hizo.
Mbio hizo zinalenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za Afya zilitambulishwa katika nyumba ya kulala wageni ya Kia iliyopo Mkoani Kilimanjaro na Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Jairy Khanga.
Akizungumza Juni 12, 2022 katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Amref Health Africa, Anthony Chamungwana amesema mbio hizo za kuendesha baiskeli zilianza rasmi miaka 7 iliyopita ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia sekta ya Afya Tanzania na mafanikio makubwa yameonekana.
Aliongeza kuwa Amref Health Africa Uholanzi imekuwa ikisaidia miradi na matukio yenye athari kubwa ikiwa ni pamoja na tukio hili la kuendesha baiskeli barani Afrika ambalo hukusanya kiasi kinachoweza kudaiwa cha fedha kwa ajili ya suluhu za afya.
“Tunashukuru kwamba Amref Tanzania ni miongoni mwa wanufaika wa hazina hiyo  na tunataka kuwahakikishia kwamba, tunathamini jitihada zenu hasa mipango ya kukusanya fedha ambayo mnapigania kusaidia Waafrika kupitia afua mbalimbali za afya.” amesema Chamungwana .
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mkazi wa Amref Tanzanzia Gaspar Jonah, Ag. alisema kuwa mchezo huo umekuwa ukifanywa kila mwaka lakini kwa miaka 2 iliyopita haikuwezekana kutokana na mlipuko wa COVID-19, huku akiwapongeza , washiriki kwa kuwa na subira hadi wakati huu tena na kujitokeza kushiriki mchezo huo.
“Uongozi wa Amref unathamini Mamlaka ya Kilimanjaro kwa kujitolea na uungwaji mkono unaotolewa kwetu kila wakati, hili halingewezekana bila ushirikiano wako, tutaendelea kukuarifu na kutafuta mwongozo wako wakati wowote mpango/fursa za aina hii za kusaidia jumuiya yetu zinapotokea”. amesema Gaspar.
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi