November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nauli za Mabasi ya Mikoani ziwe rafiki kwa Wananchi

Na Geofrey J.Mlwilo (TUDARCo)

Tangu kuanza kwa Mgogogoro baina ya Urusi na Ukraine Mapema Mwaka huu 2022 Kumekua na uhaba wa mafuta dunia nzima, hii ni kutokana na wazarishaji wakuu wa mafuta yaani Urusi kuwekewa vikwazo vya uchumi ikiwa ni pamoja na Kuzuiliwa kuuza mafuta yake kwenye nchi mbalimbali.

Tukio hilo limekua ni msiba kwa nchi nyingi za bara la Africa ambao wamekua wahanga wa Vikwazo vya kiuchumi kwa nchi ya Urusi kwani gharama ya kuuza mafuta imepanda marafudu kutokana na upatikanaji wake kuwa pungufu.

Hali hii haijaiacha nchi ya Tanzania nyuma, bei ya mafuta imepanda pia hivyo kusababisha ongezeko la gharama za nauli kwa Mabasi ya mikoani na hata yale ya nnje ya nchi.

Swali kubwa lililobaki je, Wananchi wa hali ya chini na kawaida wanamudu gharama hizo za nauli? ni wazi imekua changamoto kubwa kwa wananchi hususani watumiaji wa usafiri huo hivyo ni muhimu kwa Serikali kuangalua upya bei za nauli hasa kwa mabasi ya mkoani ili kusaidia wananchi hususani wa kiwango cha chini na kawaida.

Punguzo la bei kinawezekana kama Serikali itaamua kupunguza baadhi ya kodi ili kusaidia wananchi wake kuondokana na changamoto zinazowakabili katika kipindi hiki ambacho gharama za maisha zinapanda kutokana na uhaba wa mafuta.