Na Mwandishi wetu ,Timesmajira Online,Dodoma
MBUNGE wa jimbo la Lupa wilayani Chunya Mkoani Mbeya , Masache Kasaka ameiomba serikali kuboresha mawasiliano ya mtandao wa simu katika vijiji vya Shoga,upendo pamoja na Sipa kutokana na changamoto hiyo kuwepo kwa muda mrefu .
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lupa ,Waziri wa Habari mawasiliano na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa mwaka huu wa fedha wametenga minala mingi kidogo lakini kwa maana eneo maalum anakotoka Mbunge huyo kuwa na shughuli za kiuchumi zilizopo katika maeneo hayo watazipa kipaumbele cha peke yake .
Hata hivyo Mhe. Nnauye amesema kama katika orodha walizotoa wakati wa bajeti hizo kata na maeneo yaliyotajwa hayamo basi nao wataingizwa kwenye orodha yale maeneo maalum kwasababu ya shughuli nyingi za kiuchumi kufanyika kwenye maeneo hayo .
Aidha Mh. Nnauye amesema kuwa serikali ipo tayari kusaidia kushirikiana ujenzi wa uchumi wa kidigitali ili uweze kuingia uchumi wa jumla .
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini