Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga(Tanga Uwasa) imewataka wakazi wa jiji laTanga kutembelea banda lao ili wapate kujua huduma za maji zinavyotolewa kupitia mkataba wa huduma kwa wateja.
Tanga Uwasa ilifanya maboresho ya mikataba na sasa wanaiwakilisha kwa Wananchi kuijua Tanga UWASA ina majukumu gani na inafanya nini katika kuhakikisha mwananchi anapata maji safi na salama.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devotha Mayala wakati wa Maonyesho ya 9 ya Biashara na utalii yanayofanyika mkoani Tanga.
Afisa uhusiano huyo amesema kuwa kitendo cha wakazi wa jiji la Tanga kuwatembelea kitasaidia kuwapunguzia nalalamiko kwani kila mteja atapata nafasi ya kupata elimu kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kusoma mita zao za maji.
“Mwaka huu tunatumia maonyesho haya kuja kuwakabidhi watu mikataba ya huduma kwa mteja,tulifanya maboresho kwenye mkataba wetu tuliokuwa tunatumia sasa uneshakamilika na sasa tunawakilisha kwa wateja wetu,”
Na ndani ya mkataba wa huduma kwa mteja tumeainiasha Tanga Uwasa ni nini,inafanya nini,iko wapi,na kwa sasa tunafanya huduma za kusambaza maji Tanga jiji,Muheza na Pangani”alisema Mayala
Aidha ameongeza kuwa katika banda lao wameweka huduma zote ambazo mwananchi ataweza kujua namna mchakato wa maji unavyofika mpaka nyumbani
“Kwenye banda letu kuna wataalamu kutoka vitengo mbalimbali,huduma kwa wateja kama una maswali yeyote unaweza kupata majibu hapahapa”alisema Mayala
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo walionyesha kufurahishwa na huduma zinazotolewa huku wakiwahamasisha wakazi wa jiji la Tanga kuacha kujifungia majumbani na badala yake watoke ili waweze kupata elimu itakayowasaidia kuacha kulalamika kila wakati.
More Stories
Rehema Simfukwe atoboa siri sababu kuimba wimbo wa Chanzo
Tanzania ipo tayari kupokea wakuu wa nchi,mkutano wa nishati-Dkt.Kazungu
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano