November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya EQUITY yazindua tawi Kahama

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Kahama

Serikali wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imetoa ushauri  wakulima , wajasiriamali wadodo , wa kati na wakubwa kuchangamkia   fursa za uwekezaji unaofanywa  na taasisi za fedha wilayani hapa ziweze kuwanufaisha  kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Ushari huo umetolewa na katibu tawala wa wilaya ya Kahama , Timothi Ndanhya kwenye uzinduzi rasmi wa  benki ya EQUITY tawi la Kahama na kuwataka watu hao  kuchangamkia  fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotolewa na taasisi za fedha , mabenki katika  kujiletea maendeleo.

Ndanhya alisema wilaya ya Kahama ina bahati ya kuwepo na taasisi nyingi za kifeza kwa kuwa na matawi 12 ya benki yaliyofunguliwa katika wilaya ya Kahama na yamukuwa yakitoa  fursa mbalimbali za kiuchumi na kuwataka  kuzitumia ziweze kuwasaidia kukuza mitaji yao na kujiletea maendeleo.

Awali katika hotuba yake kaimu mkurugenzi mtendaji wa EQUITY  benki Tanzania, Betty Kwoko alisema benki yao ni biashara katika malengo yake , lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya kila Mtanzania kiuchumi na jamii.

Kwoko alisema benki ya EQUITY ni miongoni mwa taasisi bora ya fedha katika kutoa huduma bora kwa wateja wake na kwa wafanyabiashara wadogo , wa kati na wakubwa na kutokana na utafiti wake wilaya ya Kahama yenye halmashauri tatu inamalengo ya kibiashara katika kukuza uchumi wa wananchi wake.

Alisema katika mpango wa mkakati wa Benki ya EQUITY  wa miaka mitano  wameweka malengo sawa na ya serikali ya wilaya ya Kahama kuhusu biashara ya Madini ya dhahabu , Almasi na kwa upande wa kilimo cha mazao ya Pamba , Tumbaku , Alizeti , Choroko , Degu kuhakikisha wanawasaidia kiuchumi wanaofanya shughuli hizo.

Kwoko alisema katika mpango huo pia wamejumuisha pamoja na wajasiriamali wadogo , wa kati na wakubwa wamewajumisha kwenye vipaumbele vya benki hiyo na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma mbalimbali zitakazotolewa pamoja na fursa ya kupata elimu bule ya fedha na uwekezaji wa amana , utuzaji wa fedha  na mikopo nafuu kwa ujasiriamali  mdogo , wa kati na mkubwa.

Nao wananchi na wateja waliofika kwenye uzinduzi huo John Manjale na Delfine Kalunde walipongeza mpango mkakati wa benki hiyo katika kuwasaidia watu  wa kada zote za kiuchumi ziweze kuwasaidia  kubadilisha maisha na kujiletea maendeleo.

Meneja wa tawi la benki ya EQUITY la wilaya ya Kahama Beatus Tesha akiongea wakati wa ufunguzi wa benki hiyo wilayani Kahama
Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa Taifa wa benki ya EQUITY , Betty Kwoko akitoa hutuba wakati wa ufunguzi wa tawi la benki hiyo wilayani Kahama.
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa tawi la Benki ya EQUITY tawi la Kahama, afisa tawala wa wilaya ya Kahama , Timothi Ndanhya akitoa hutuba yake kwenye ufunguzi wa tawi la benki hiyo mjini Kahama .
Katibu tawala wa wilaya ya Kahama , Timothi Ndanhya katikati akifungua rasmi tawi la Benki ya EQUITY tawi la Kahama kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa taifa wa benki ya EQUITY ,Betty Kwoko na kulia ni meneja wa tawi hilo Beatus Tesha , picha zote na Patrick Mabula.
Meneja wa  benki ya EQUITY tawi la wilaya ya Kahama, Beatus Tesha wa kwanza kushoto akieleza namna walivyojipanga kutoa huduma kwa wateja baada ya ufunguzi rasmi wa tawi la benki hiyo wilayani hapa wa pili ni mgeni rasmi katika ufunguzi huo Timothi Ndanhya na watatu toka kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa taifa wa benki hiyo Betty Kwoko , Picha na Patrick Mabula
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa taifa wa benki ya EQUITY , akieleza utoaji wa huduma kwa wateja ndani ya benki hiyo tawi la wilaya ya Kahama baada ya ufunguzi rasmi katikati ni meneja wa tawi la benki hiyo wilaya ya Kahama Beatus Tesha, na kulia ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo katibu tawala wa wilaya ya Kahama , Timothi Ndanhya.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye ufunguzi wa benki ya EQUITY Tawi la wilaya ya Kahama
Wafanyakazi wa benki ya EQUITY wakiwa na mgeni rasmi katibu tawala wa wilaya ya Kahama ,Timothi Ndanhya aliyesimama katikati baada ya kufungua rasmi tawi la benki hiyo wilayani Kahama