November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Utendajikazi wa Rais Samia wamkumbusha Rais Sirleaf

Na Mwandishi Wetu, TimesMajiraOnline

RAIS Samia Suluhu Hassan aliingia madarakani Machi 2021, huku uongozi wake ukiwa ni alama ndani ya mwaka mmoja ulileta tofauti kubwa katika taifa la Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa zamani wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf alisema kuwa kuingia kwake madarakani kulifungua mlango wa majadilaino kwa wapinzani.

Kuingia kwake madarakani kumejenga imani katika mfumo wa kidemokrasia pia jitihada zake zimefanywa kuongeza uhuru wa habari, pamoja na wanawake na wasichana kuwa na mfano mpya wa kuiga.

Septemba 2021, ikiwa ni mwezi mmoja toka awe Rais, Samia alihutubia akiwa ni mwanamke wa tano Mwafrika kuwahi kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

“Alisimama pale ambapo mimi niliwahi kusimama miaka 15 iliyopita nikiwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais mwanamke katika uchaguzi wa kidemokrasia barani Afrika.

“Kama Rais wa kwanza mwanamke katika historia nchini kwangu” alisema, “mzigo wa matarajio ya kufikia malengo ya usawa wa kijinsia ulikuwa ni mzito sana katika mabega yangu” ilisema sehemu ya taarifa yake.

Alisema kuwa alishindwa kujizuia kufikiria jinsi mabega ya kiongozi mwanamke na uwezo wa kuleta tofauti.

Sirleaf alikuwa Rais wa Liberia na mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel.