Na Penina Malundo, TimesMajira,OnlineĀ
MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini, Mariam Ditopile ameimpongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Samia Suluhu Hassan kwa kutenga bajeti ya kilimo inayokwenda kufanya mapinduzi kwenye sekta hiyo.
Ditopile amesema hayo leo Jumatano Mei 17, 2022, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo yam waka 2022/23 ya Bilioni 1751.12 ikiwa imeongezeka kutoka bilioni 294.16.
Akichangia bajeti hiyo, Ditopile amesema, kwa kipindi kirefu bajeti ya kilimo imekuwa ikilalamikiwa na wabunge kwamba ni kidogo lakini mwaka huu imepanda huku akimpongeza Rais Samia kwa kuwateua Bashe kuwa waziri na Anthony Mavumbe kuwa naibu ambao wanaonesha mwanga kwenye sekta hiyo.
“Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia kwenye nchi yetu hii ni bajeti ya kwanza inaletwa na Serikali na hakuna mtu analalamika kwamba ni ndogo hapa nimpe pongezi Rais Samia Suluhu Hassan kwa hakika ameonesha yeye ni mkulima mwenzetu na anajali kwa vitendo maslahi ya wakulima nchini na hilo amedhihirisha kwa kutuletea waziri na naibu wake wenye kujali wakulima,” amesema Ditopile
Amesema kilimo kinafanyika sana nchini, ndio maana katika takwimu za Serikali tunaelezwa kilimo kimeajiri asilimia kubwa ya Watanzania, lakini cha kushangaza mkulima anakutana na serikali baada ya kuvuna.
āKilimo ni utafiti na utaalamu, ni udongo ama mbegu, ni sayansi na teknolojia, ni dawa, ni maji kwa maana ya mvua au umwagiliaji, ni miundombinu ya uvunaji, ni urutubisho, ni uhifadhi na ni soko na ukikosoea jambo moja umeondoa tija kwenye kilimo,ā amesema Ditopile
Mbunge huyo kutoka Mkoa wa Dodoma amesema wasiache sayansi na teknolojia, waende sawa na dunia.”kwa nini tunakataa mbegu za GMO, tunazikataa kwa nini, tunalima Pamba tunataka kuzalisha nguo, lakini Brazili, India na China wanatumia GMO, sisi tunachokitaka tuleteeni na mkulima aamue, mnasema zina madhara ni uongo mtupu.āamehoji
Aidha, Ditopile amezishauri wizara ya kilimo kufanya kazi kwa ukaribu na wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara ili kuwezesha kuwasaidia wakulima kulima mazao yenye tija kwa kipindi fulani.
āNishauri kwamba, tuanzie sokoni, leo hii uhaba wa mafuta ya kula umekuja kujulikana kupitia viwanda vya kibiashara. Niombe wizara ya kilimo na ya biashara mkae pamoja na kushirikiana ili kuwashauri wakulima walime mazao gani yenye tija kwa musimu husikakuwa,ā amesema Ditopile na kuongeza:
āBajeti ya kilimo imepanda, niliwahi kushauri vijana lazima watengenezewe namna ya kushiriki kwenye kilimo, naona kundi kubwa hili ambalo nimekuwa mtetezi wao mmewakumbuka na mnakwenda kutoa vitendea kazi na watashiriki sasa kwenye kilimo.āamesisitiza
Amesema Bajeti ya kilimo imepanda na imeikumbuka kundi ya vijana lazima watengenezewe namna ya kushiriki kwenye kilimo.” naona kundi kubwa hili ambalo nimekuwa mtetezi wao mmewakumbuka na mnakwenda kutoa vitendea kazi na watashiriki sasa kwenye kilimo,”amesisitiza Ditopile
Bajeti ya Kilimo iliwasilishwa jana Jumanne na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 155.34 ambapo sehemu kubwa ya fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na miundombinu ya uhifadhi wa mazao.
Pia, kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao, kuimarisha utafiti wa kilimo, uzalishaji wa mbegu na utoaji wa ruzuku.
More Stories
Bumbuli kutekeleza miradi kwa kuangalia vipaumbele
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani