November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makalla: Mgogoro wa ardhi Mbondole Chanika busara zinahitajika

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla Jumatatu ya May 09 anatarajia kufika eneo la Mbondole Kata ya Chanika kwaajili ya kutafuta maridhiano na Suluhu ya Kumaliza Mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 ukihusisha Wakazi 700 waliovamia na kujenga zaidi ya Nyumba 200 kwenye eneo la Mwananchi aliefahamika kwa majina ya Martin Nasson aliekuwa ametenga kwaajili ya Ujenzi wa Shule.

Mapema Leo RC Makalla amefanya kikao Cha pamoja baina yake na Walalamikaji, Walalamikiwa, Kamati ya Ulinzi na usalama, Wataalamu wa Ardhi kwa lengo la kuangalia Busara inayoweza kutumika kumaliza Mgogoro huo kwa amani na usalama licha ya Mahakama kutoa hukumu ya haki kwa mmiliki halali wa eneo na kuamuru wavamizi waondolewe.

Kutokana na Mgogoro huo kuhisisha familia nyingi, RC Makalla ameona ni vyema kabla ya kutekelezwa kwa hukumu ya Mahakama kukaangaliwa Njia ya Busara ya Kumaliza Mgogoro ikiwemo Wavamizi kumlipa fidia Mmiliki halali ili waweze kusalia kwenye eneo endapo mmiliki atakubali ombi Hilo.

RC Makalla amesema katika kikao Cha Leo Baada ya kusikiliza pande zote mbili amebaini dosari mbalimbali ikiwemo mmiliki halali kutishwa na wavamizi na kutopewa haki kufika kwenye eneo lake na kutopatikana kwa takwimu kamili ya idadi ya wavamizi.

Jambo hilo limemlazimu RC Makalla kutenga siku ya Jumatatu saa nne asubuhi kufika eneo la tukio ambapo ameelekeza kila mvamizi kusimama kwenye eneo analodai ameuziwa Akiwa na Nyaraka zote za mauzio ili kupata tarifa sahihi.

Pamoja na hayo RC Makalla amewatahadharisha Wananchi kuacha tabia ya kuvamia na kujenga kwenye maeneo ya watu na kuzielekeza Taasisi na watu binafsi kuyalinda na kuyaendeleza Maeneo.