Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Tigo wameshinda Tuzo ya Usalama na Afya Mahali pa kazi inayotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali (OSHA) Jijini Dodoma. Tuzo imekabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.
Tigo wanatambua umuhimu wa usalama na afya mahali pa kazi mara zote. Hivyo basi wamefanya tathimini ya usalama wa wafanyakazi wetu mahali kwa kazi ili kuendelea kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja wao mara zote.
Pia Tigo wamesema watahakikisha, wanaelimisha na kuhamasisha masuala ya Usalama na Afya Mahali pa kazi pamoja kwa kuweka mifumo thabiti itakayo zuia ajali kwa kuchukua tahadhali mapema, magonjwa na vifo pamoja na uharibifu wa mali ikiwa lengo ni kupunguza gharama za uendeshaji nk
Kauli Mbiu ya Mwaka 2022: Act Together to build Healt and Safety Culture.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati