October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Korea Kusini katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona kwa wanafunzi

Korea Kusini yafunga shule tena, Corona yaibuka upya

SEOUL, Zaidi ya shule 200 nichini Korea Kusini zimelazimika kufunga tena zikiwa ni shule siku chache baada ya kufunguliwa, kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Jumatano iliyopita melfu ya wanafunzi walirejea shuleni baada ya kufunguliwa tena nchini humo na kulegeza masharti yaliyowekwa awali kukabiliana na virusi vya corona .

Kwa mujibu wa Gazeti la Korea Times,baada ya siku moja tu, maambukizi mapya 79 yalirekodiwa, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kwa siku nchini humo kwa kipindi cha miezi 12.

Wakati huo huo, ghala lililopo mji wa Bucheon, linaloendeshwa na kampuni kubwa ya kibiashara ya Coupang, na maafisa walisema sehemu hiyo ilikuwa haitekelezi kikamilifu hatua za kuzuia maambukizi.

Aidha, wachambuzi wa masuala ya afya wanaeleza inawezekana Korea Kusini ikaendelea kurekodi maambukizi mapya wakati huu inapoendelea kupima maelfu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Maambukizi mapya 58 yalirikodiwa siku ya Ijumaa, na kusababisha taifa hilo kuwa na jumla ya idadi ya watu wenye maambukizi ya corona 11,402.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Wizara ya Elimu imesema jumla ya shule 117 katika mji mkuu wa Seoul pia zimeahirisha tarehe ya kufunguliwa tena kwa shule.

Mwanafunzi mmoja mjini Seoul ambaye mama yake alikuwa akifanya kazi katika ghala la kampuni ya Coupang pia naye alipatikana na na virusi vya corona.

Wakati huo huo, idadi ya waliokufa kutokana na virusi vya corona nchini Brazil imefikia watu 28,834 ikiizidi ile ya Ufaransa na kuwa taifa la nne duniani kwa idadi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na janga la COVID-19.

Wizara ya Afya nchini humo ilieleza taifa hilo ambalo sasa ni kitovu cha virusi vya corona katika eneo la Amerika ya Kusini, limerikodi visa vipya 33,274 vya maambukzi katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Miji ya Sao Paulo na Rio de Janeiro ndiyo imeathriiwa zaidi nchini Brazil kwa kuwa na idadi kubwa ya visa vya maambukizi huku maeneo masikini ya Kaskazini na Kaskazini Mashariki ya nchi hiyo yakishuhudia pia wimbi kubwa la wagonjwa.

Janga la COVID-19 linasambaa nchini Brazil chini ya kiwingu cha kutunishiana misuli kati ya magavana na mameya wanaotekeleza hatua kali za vizuizi na Rais Jair Bolsonaro anayepinga hatua hizo kwa sababu za kiuchumi.