November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampeni ya Mwa Mwii na Tigo pesa yaongeza idadi ya watanzania kufanya malipo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni ya mawasiliano ya simu Tanzania-TIGO imesema kupitia kampeni yake ya mwa mwi imeweza kuongeza idadi ya watanzania wanaofanya malipo ya serikali na bidhaa mbalimbali kwa njia ya kidigitali ikiwa Dunia inaelekea kwenye uchimi wa kidigitali.

Akizungumza Leo jijini dar es salaam wakati wa kuendesha droo ya 3 na ya 4 ya kampeni hiyo Meneja wa kitengo Cha wateja wathamani ya juu wa TIGO PESA, Mary Rutta amesema kupitia kampeni hiyo hadi sasa wametoa kiasi Cha shilingi milioni 160 Kwa wateja wa tigo wanaofanya miamala mbalimbali kupitia huduma ya TIGOPESA

“Tumefikia wiki ya nne ya Kampeni yetu ya pesa mwa mwi ambapo tumeweza kupata washindi wa droo ya 4 ambao wote wamejishindia shilingi Milioni 2, washindi wametoka sehemu mbalimbali Tanzania lakini Kuna ambao wameweza kufika makao makuu kwaajili ya kupokea zawadi yao”

“Mpaka sasa muitikio ni mkubwa, wateja wengi wameongezeka kufanya miamala ya tigo pesa hasa miamala ya lipa kwa simu na malipo ya bili kama vile malipo ya serikali”

Aidha Mary amesema hii ni wiki ya mwisho ya kufanya promotion ya pesa mwa mwii hivyo anewasihi wateja wa Tigo pesa waendelee kufanya miamala mpaka tarehe 17 ambayo ndiyo mwisho wa Kampeni ili waweze kuingia kwenye droo ya mwisho itakayofanyika wiki ijayo ya kutafuta washindi wa wiki ya Tano pamoja na wale washindi wakubwa watakojishindia Milioni 10 kila mmoja na mshindi mmoja atakayejishindia shilingi Milioni 25

Pia amesema promosheni hiyo ya wiki sita inayomalizika wiki ijayo maalum kwa wateja wa Tigo Pesa washindi 10 wa droo ya mwisho Kila mmoja atapata zawadi ya shilingi milioni 10 na mshindi 1 wa jumla atapata shilingi milioni 25.

“Fanya miamala ya TigoPesa, lipa bili, tuma pesa kwa mteja wa Tigo pesa aliyesajiliwa, pokea pesa kutoka mitandao mingine na pia tumia lipa kwa simu au fanya malipo ya serikali ili uingizwe kwenye droo ya mwisho ya kutafuta washindi wa Milioni 2 na mshindi wa Milioni 10 na pia mshindi wa milioni 25”

Kwa upande wake Mshindi wa Kampeni hiyo ya pesa mwa mwii, Neema Thomas Towo, alisema yeye ni mteja wa Tigo na ameshinda pesa hizo kwa kufanya miamala mbalimbali kwa kulipa bili, luku na kufanya manunuzi binafsi kwa kulipa kutumia tigo pesa hivyo amewashauri watanzania waendelee kutumia TigoPesa ili waweze kuwa washindi wa droo za wiki

Naye Abdallah Frank ambaye ni mshindi wa Kampeni hiyo ya Pesa Mwa Mwii, amesema amefurahi kwa kuwa mshindi wa shilingi Milioni 2 na pesa hizo atazitumia katika kujiendeleza kwenye biashara zake anazozifanya.