Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo watoa misaada mbalimbali ya vyakula na vifaa vya Shule kwa Wanafunzi wa shule ya Msingi Bangulo Gongolamboto Wilaya ya Ilala.
Misaada hiyo ulitolewa shuleni hapo katika siku Maalum ya matendo mema Duniani ambapo Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo kila mwaka imetenga siku hiyo kutoa misaada kwa makundi maalum pamoja na Wanafunzi wenye Mazingira magumu.
Akizungumza shuleni hapo mara baada kutoa msaada huo Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau, alisema madhimisho ya siku ya matendo mema Duniani kwa Wilaya ya Ilala yatadhimishwa wiki hii ukumbi wa John Bosco Upanga kabla kufika siku hiyo wanatoa chochote walichojaliwa kwa Jamii.
“Fahari Tuamke Maendeleo Leo tumetoa msaada shule ya Msingi Bangulo Gongolamboto misaada tuliotoa Leo kwa wanafunzi wenye Mazingira magumu Vifaa vya shule daftari ,Viatu kila mwanafunzi pamoja na unga wa sembe ” alisema Neema
Neema mchau alisema Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo ni Taasisi ya kijamii inashirikiana na Serikali katika Shughuli mbalimbali ikiwemo kuwekeza sekta ya Elimu Wilaya ya Ilala.
Alisema Fahari Tuamke Maendeleo tumejenga tabia kila mwaka tunasaidia jamii aidha sekta ya elimu na makundi maalum.
Alisema shule Msingi Ulongoni Gongolamboto ina wanafunzi waliopo katika Mazingira magumu kutokana na Wazazi wao kukosa uwezo wa Vifaa vya shule ikiwemo daftari,sare za shule ,viatu Fahari Tuamke Maendeleo imekuwa mlezi wa Wanafunzi hao katika juhudi za kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA kuwapatia vifaa vya Shule Ili washike elimu ije kuwakomboa
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini