Na Mwandishi wetu, TimesMajira Updates
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana leo tarehe 05 April, 2022 amekutana na Wataalamu kutoka Idara ya Wanyamapori kwa lengo la kupata uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya Sekta ya Wanyamapori nchini .
Katika Kikao hicho Waziri Dkt.Pindi Chana amewasisitiza watalaam hao wafanye kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ili kuboresha Sekta hiyo kwa kuvutia Watalii na kuongeza Pato la Taifa hususani katika kipindi hiki ambacho tasnia ya utalii imeathiriwa na janga la UVIKO 19

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha pamoja na Wataalamu mbalimbali kutoka idara ya Wanyamapori.
More Stories
Lushoto watakiwa kumuunga mkono Rais Samia kuimarisha elimu
Zaidi ya bilioni 100 zatolewa kwa ajili ya madaraja 13,Lindi
Serikali kupeleka milioni 100 kwa ajili ya kituo cha afya Saranga