November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Bashe na mkakati wa serikali juu ya uanzishwaji wa Benki za mbegu asili za kilimo

Na David John TimesMajira Online

KILIMO ni uzalishaji wa Mazao kwenye mashamba na kinamaana pana inayojuimuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji,wa wanyama na uvuvi wa samaki majini.

Sekta ya Kilimo ni muhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za nje ya nchi pia.

Eneo hili la kilimo kwa tafiti mbalimbali limeweza kuajiri zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote nchini na kuzalisha mazao ya chakula na biashara.

Mazao makuu ya chakula ya aina ya wanga yanayozalishwa nipamoja na mahindi, muhogo, mpunga na mtama na. Mazao mengine ni ndizi, viazi vitamu na viazi mviringo, ngano, ulezi pamoja na uwele.

Mazao ya mikunde ni pamoja na maharage, kunde, mbaazi, choroko na njegere. Mazao yote hayo ndiyo yanayochangia taifa kujitosheleza kwa
chakula kwa zaidi ya asilimia 100.

Mazao makuu ya biashara ni korosho, miwa kwa ajili ya sukari, pamba, mkonge, tumbaku, pareto, kahawa na chai na mengine ni ya bustani na mbegu za mafuta.

Pamoja na kujitosheleza kwa chakula na kuchangia katika uchumi wa taifa, takriban mazao yote yamekuwa yakizalishwa kwa tija ndogo kwa maana ya kiasi cha mazao yanayozalishwa
kwa eneo.

Pia uzalishaji umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya mazao hayo kuzalishwa katika maeneo yaliyo nje ya ikolojia yake ya asili.

Imekuwa ni sababu mojawapo kwa baadhi ya maeneo nchini kuwa na tija ndogo na upungufu wa mazao ya chakula na biashara. Uzalishaji wa mazao nje ya ikolojia yake ya asili
hupelekea kuwa na tija ndogo na au kuyazalisha kwa gharama kubwa kama vile umwagiliaji maji.

Hata hivyo leo tunataka kuangazia kwa habari ya mbegu kwa maana kuna mfumo wa mbegu rasmi na ule ambayo si rasmi ambapo mfumo rasmi ni ule ambao mkulima anaweza kutuza mbegu kwa ajili ya msimu unaofuata.lakini mfumo mungine ni ule mkulima ananunua mbegu madukani.

Hata hivyo kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na changamoto kubwa ya wakulima kujenga tamaduni ya kutuza mbegu za kilimo na badala yake wamekuwa wakitumia mfumo wa kununua madukani jambo ambalo limepunguza ufanisi mkubwa kwenye uzalishaji.

Licha ya kwamba eneo la kilimo limeajili Idadi kubwa ya watanzania na limekuwa likichangia pato kubwa kwenye uchumi wa Tanzanian lakini moja ya changamoto ambayo wanakutana nayo wakulima ni mbegu.

Kutokana na changamoto hiyo ambayo ilipelekea Serikali kupitia Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kutanga Rasmi kwamba serikali itaazisha Benki Kubwa ya mbegu za kilimo ambayo itarudisha misingi na uasili wa kilimo nchini kwa wakulima kuwa na mahala maalumu pa kupata mbegu.

Bashe ambaye sasa Waziri kamili wa Wizara hiyo pia amesema pamoja Na uazishwaji wa benki hiyo ya mbegu za asili ambayo msingi wake ni kuhifadhi mbegu hizo ambazo zitatumika mashambani kwa ajili ya kilimo nakusisitiza kwamba mazao yatokanayo mbegu za asili hata soko lake ni Kubwa.

Waziri Bashe kupitia mkutano ule wa pili wa kongamano la kilimo hai alitanabaisha kwamba kuazisha benki hiyo lengo nikutaka kuzalisha kwa wingi mbegu za asili kwani bila kufanya hivyo miaka michache ijayo mbegu hizo zinaweza kupotea Kabisa.

Pamoja na mambo mengi Waziri Bashe amesema Wizara yake itaazisha kitengo maalumu kitakachoshughulikia masuala ya kilimo hai ambapo katika mwaka wa fedha wa 2022 kwenye bajeti watakitengea fedha.

Abdallah Mkindi yeye ni mdau wa mbegu za asili lakini mratibu wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kilimo Hai(Tabio)anasema Benki za mbegu za jamii ni taasisi zisizo zisizo rasmi zinazoongozwa na kusimamiwa na wakulima au serikali za mitaa, ambapo kazi ya msingi ni kuhifadhi mbegu kwa ajili ya matumizi ya ndani.

Anasema benki hizi zinapatikana katika maeneo mengi duniani na zimekuwepo kwa miaka mingi zikiwa na lengo la kuhifadhi,kurejesha,kuimarisha,na kuboresha mifumo ya mbegu ya ndani.

Hapa nchini mwamko wa wanajamii kuanzisha na kusimamia benki za mbegu ni mdogo benki hizi zilikuwa zinapatikana katika maeneo machache ya Dodoma na mbeya. Benki hizi zinajulikana kwa majina mbalimbali.:

Benki za jeni za Jamii,nyumba za mbegu za wakulima, vibanda vya mbegu, vikundi vya kutunza mbegu, ushirika au mtandao wa kutunza mbegu, hifadhi ya mbegu za jamii,maktaba ya mbegu na benki ya mbegu za jamii.

Amesema wakulima wanaoendesha benki za mbegu jamii huhifadhi mbegu za mazao ya aina mbalimbali zikiwemo zile zinazolimwa kwa wingi mfano Mahindi ,Mpunga, pia wanahifadhi mbegu za mazao yanayolimwa kwa uchache Kama vile mtama na mazao ambayo walaji wameyatekeleza Kama vile viazi vikuu. Mbegu hizi zinaweza kuhifadhiwa kwa kiasi kidogo au kikubwa kulingana na hitaji na upatikanaji.

  Kuhusu kazi za benki za mbegu

Kutoa Elimu na kuongeza ufahamu wa maswala yanayohusu mbegu ,uhifadhi wa taarifa na maarifa ya asili ya mbegu

Hatua za Mchakato wa Kuazisha na kusaidia Benki za Mbegu za Jamii

Kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa kujengwa uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kuanzisha na kusimamia benki ya mbegu. Miundombinu kwa ajili ya kuhifadhi mbegu ije baada ya jamii kuwa na uelewa wa kutosha na kuwa tayari kuansisha na kusimamia benki husika.

kuwa na jengo zuri peke yake kwa ajili ya benki ya mbegu haifai ikiwa wakulima hawana Motisha na ujuzi wa kulitumia lakini pia kuna hatua tisa kuu katika kuanzisha na kuunga mkono benki ya mbegu ya jamii.

Hatua ya Kwanza ni uchambuzi wa hali halisi ya mbegu ambapo hatua hiyo inahusisha shughuli tatu ,uchambuzi wa Mazao,uchambuzi wa mwenendo wake,mifumo ya mbegu na uteuzi wa jamii na sehemu au eneo la kuazishia benki ya mbegu.

Pia kuchagua aina za mbegu kwa ajili ya kuhifadhi, kuchagua mbegu bora,kuingiza taarifa za mbegu kwenye daftari la kumbukumbu benki za mbegu za jamii siyo tu kuwa ni sehemu ya kuhifadhi mbegu na vipando lakini pia ni sehemu ambayo ujuzi wa asili na taarifa husika kuhusu mbegu za asili zinaweza kuptikana ni Muhimu wakulima wakafundishwa kuweka taarifa za mbegu kwenye benki

Miongoni mwa taarifa hizo ni jina la mbegu la asili au la kisayansi, matumizi yake maalum, hali ya sasa ya upatikanaji wa mbegu hiyo, sifa za jumla za mbegu hizo,mbinu za kulima mbegu hizo, kiwango cha usambazaji wa kilimo chake,uwezo wake wa kuvumilia magonjwa, ukame, thamani ya lishe yake pamoja na matimizi mbalimbali ya mbegu hiyo.

Hata hivyo Mkindi Anasema kamati ya utendaji ya benki ya mbegu ya jamii nikufanya maamuzi ya kupendekeza namna mbegu zitakavyokusanywa kutoka wanachama au wakulima, kuhakikisha kuwa mbegu zinazokusanywa ni zile bora zisizokuwa na magonjwa, Magugu, wala wadudu lakini mwisho ni kukusanya taarifa za mbegu.

K. uhusu kushirikisha habari na uzoefu kati ya wanachama, wasio wanachama na wadau wengine ni jukumu jingine muhimu la benki za mbegu za jamii, kushirikishana huku kunaweza kufanyika kwa kuanda matukio ya misimu ambapo wakulima hubadilishana mbegu za maarifa yanayohusiana na mbegu.

Pia vilevile vikundi vya wakulima vinaweza kutenga baadhi ya siku za kutembelea mashamba ili kujionea aina mbalimbali za mbegu zinazopandwa, kutumia fursa za mikutano ya kijiji na mingineyo katika kupashana habari zinazohusiana na benki za mbegu.