November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Nissan nchini Tanzania yazindua gari jipya aina ya Navana SC

Na Penina Malundo,TimesMajira,Online

MIONGONI mwa  Changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wengi wanaoingiza magari nchini ni pamoja na uwekaji wa mafuta machafu ambao   unaoathiri mfumo wa injini katika magari mengi na kusababisha gari kuonekana bovu.

Akizungumza hayo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Magari aina ya Nissan Tanzania,Mark Van Rooyen wakati wa uzinduzi  wakati wa uzinduzi wa gari mpya aina ya Navana SC  yanayoingizwa na kampuni hiyo ya Nissan .

Amesema mara nyingi magari yanapoingia nchini yanakuwa hayana itilafu ila nafuta yanayowekwa katika magari hayo yanakuwa ni miongoni mwa Changamoto  ya kusababisha ubovu katika injini.

Rooyen amesema gari hilo jipya lililozinduliwa ni miongoni mwa magari yao ambayo yanafaa katika shughuli mbalimbali hususani zile za kubeba mizigo.”Hii gari ni jipya nchini na sisi ndo wa tuliochelewa kuliingiza nchini tayari nchi kama Kenya ilishaingiza gari kama hilo ni miongoni mwa magari mazuri ambayo ni imara na ni mazuri katika kutumia  hasa shughuli za kubebea mizigo,”amesema na kuongeza kuwa

“Mwaka huu tumeleta gari hili ambapo  bei yake ni Milioni 63 ambapo tutatoa services ya gari bure kwa miaka  miwili na tunatoa dhamana  ya miaka mitatu kwa mtu atakaenunua gari hiyo,”amesema

Aidha amesema  gari hilo lililozinduliwa ni la kwanza kuwepo hapa nchini hivyo aliwaomba watanzania kuchangamkia fursa ya kununua gari hilo kwani ni la viwango vya juu

Rooyen amesema kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza magari yenye ubora wa kukidhi viwango vya juu ambapo pindi mtu anapotumia magari hayo hawezi kununua mara kwa mara.

“Leo tunazindua gari aina ya Nissan Navara SC  ambapo  gharama zake ni nafuu  kila mtanzania anauwezo wa kumudu, na kumuwezesha kufanya shughuli zake kutokana na kuwa na ubora halisi “amesema

Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Alfred Minja amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya Mapinduzi makubwa katika Sekta usafirishaji kwa kutengeneza magari ambayo yanaubora wa kutosha.

Amesema kutokana na matumizi ya kila siku gari aina ya Nissan Navara SC itamsaidia muhusika kusafiri salama na kufanya kazi zake bila wasiwasi aina yoyote.

“Kupitia usafiri huu wa gari aina ya Nissan Navara SC  mtumiaji atapata fursa kufanya shughuli zake kwa ubora pasipo kuwa na wasiwasi wa aina yoyote kwani imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu”amesema