November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt Doroth: Msifumbie macho vitendo vya ukatili, toeni taarifa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WAZIRI wa Maendeleo ya Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dk.Dorothy Gwajima ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa kwani hakuna mkatili atakaye achwa na mkono wa sheria.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo katika ziara ya kikazi katika kituo Cha Mkono kwa Mkono kilichopo Kituo Cha Afya Chanika Jijini Dar es Salaam Dk.Gwajima alisema viongozi wa dini na watu mbalimbali watumie nafasi zao kusema na jamii ili kuepuka vitendo vya ukatili.

“Wananchi mjitokeze kutoa taarifa za ukatili mje sasa kutumia hizi huduma wakatili acheni ukatili ili maisha yako yawe mazuri inategemea unaushije duniani mimi sijui kwanini unafanya ukatili hilo sio jambo jema hakuna mkatili atakaye achwa na mkono wa sheria”

“Usibebe uchungu moyoni mwako hakuna jambo ambalo halina suluhu chini ya jua ni wewe mwenyewe umeamua kujifunga mkataba na shetani jibariki mwenyewe na Mungu atakubariki” alisema

Dkt Gwajima alisema a Wizara yake itashirikiana na Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni na Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene ili kuongeza maaskari na wanasheria wengi zaidi katika madawati ambao watatoa huduma kwa wananchi

Amesema serikali itaangalia namna ya kuboresha miundombinu na majengo ya madawati ya jinsia katika Hosptali zote nchini ili kurahisisha utoaji huduma.

“Rais Samia Suluhu Hassan ameshasema tuimarishe kada na Taaluma ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii “amesema

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Ilala Dkt Elizabeth Nyemba amesema kituo Cha mkono kwa mkono kilichopo katika kituo cha afya ya chanika kilizinduliwa Novemba 24 mwaka 2020 kikiwa na lengo la kukabiliana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto( GBVNAC) ambao umekithiri katika jamii.

Amesema kituo hicho cha mkono kwa mkono kinawatumishi wa madaraja ta maafisa ustawi wa jamii, Polisi dawati la jinsia, Daktari pamoja na muuguzi.

“Kituo kinahudumia wahaga wote wa ukatili ambapo wengi wao wamekuwa wakitoka kata ya chanika, Zingiziwa, Buyuni, Majohe, Msongola, Gongolamboto pamoja na pugu.

Akitaja taarifa wahanga wa ukatili wa kijinsia katika kituo hicho kwa kipindi cha Octoba 2020 hadi Februari imefanikiwa kuwahudumia Wananchi 897.

Alisema aina za ukatili ambao umekuwa ukifanyika ni pamoja na ukatili wa kimwili 83, ukatili wa kingono 85, ukatili wa kihisia 727, ukatili wa kutelekezwa 2.