Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mardhiano ( Maridhiano Day) yanayotarajiwa kufanyika nchini kote Machi 3,mwaka huu huku lengo likiwa ni kuendelea kuhimiza amani na utulivu kwa watanzania bila kujali dini,jinsia,rangi wala itikadi za kisiasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Taifa Sheikh Alhad Mussa Salum alisema,siku hiyo itaadhimishwa katika mikoa yote nchini huku kitaifa itafanyika katika mkoa wa Dodoma .
Aidha alisema,zoezi hilo litaenda mbamba na uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto kutokana na kundi hilo kuwa miongoni mwa makundi yanayohitaji damu kwa wingi.
“Jumuiya hii ipo katika mikoa 28 hapa nchini ,hivyo siku hii itaadhimishwa nchi nzima ambapo kila mkoa utaadhimisha kwa kuchangia damu .”alisema Sheikh Salum
Sheikh Salum ambaye pia ni Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam alisema,zoezi la uchangiaji damu hivi sasa linaendelea na kwamba tayari damu nyingi imekusanywa kupitia siku hiyo.
Alisema ‘kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni ‘Tanzania ni yetu komesha mauaji dumisha upendo amani na utulivu.’
Sheikh Salum ametumia futrsa hiyo kutoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi katika tukio hilo ili kushiriana na Jumuiya hiyo katika kuadhimisha siku hiyo ya mardhiano kwa mustajabali wa Taifa la Tanzania.
Sheikh Saluma alizungumzia kuhusu ,matukio ya ukatili yanayoendelea hapa nchini ambapo alisema,Jumuiya hii imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuhakikisha amani utulivu , upendo na mshikamano vinadumishwa.
Alisema,matukio ya ukatili yanasababishwa na mambo mengi ikiwemo msongo wa mawazo,kuchanganyikiwa (inahitaji ushauri nasaha) hii inakosekana na hivyo kusababisha kukata tama,tamaa ya mali kutokana na baadhi ya watuhumiwa kuua wazazi wao ili warithi mali, magomvi na kesi za mirathi .
Hata hivyo alisema sababu yoyote haihalalishi haihalalishi kumwaga damu ya mtu mwingine huku akiwataka wananchi kukimbilia na kupelaka malalamiko yao kwenye vyombo vya sheria badala ya mtu kujichukulia sheria mkononi.
Aidha alisema,kwa upande wa Viongozi wa dini wamejiandaa kufundisha upendo,kuvumiliana na kuwa na hofu ya Mungu lakini pia kupeleka malalamiko kwenye vyomvo vya ulinzi na usalama.
xxxx
More Stories
Mwalimu adaiwa kumfanyia ukatili mwanafunzi
NAOT watakiwa kuendana na viwango vya ukaguzi
Rais Samia kuzindua mfuko wa kuendeleza kazi za wabunifu