October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wampongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua kukabiliana na ugonjwa wa corona

Na Mashaka Mhando, Tanga

 HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imempongeza Rais John Magufuli, kwa hatua alizochukua kukabiliana na ugonjwa wa Corona nchini.

Sambamba na pongezi hizo,  ugonjwa huo katika Jiji la Tanga unapungua kwa kasi kutokana na wananchi wengi kuchukua tahadhari zinazotolewa na Serikali pamoja na wataalamu wa afya. 

Akizungumza kwenye semina ya siku mbili inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga, Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga, Hamza Maulidi amesema, wananchi hawana budi kumpongeza Rais kutoka na kututoa hofu tangu alipogundulika mgonjwa mmoja hapa nchini.

Amesema, kweli ugonjwa huo bado upo nchini na wananchi waendelee kuchukua tahadhari zote pamoja na kwamba maambukizi yanashuka kwa kasi kubwa jijini hapa, lakini pia wanampongeza Rais kwa hatua alizochukua hadi ugonjwa unaendelea kupungua.

 
“Ugonjwa upo na Tanga pia upo, tuchukue hatua tunazoelekezwa na wataalamu wetu wa afya, lakini kwa kweli tunampongeza mheshimiwa Rais kwa kututia faraja tangu ugonjwa huu umeanza,”amesema Maulidi.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema yametolewa wakati muafaka ambao shughuli za kiserikali nyingi zimeanza kufanyika baada ya mikusanyiko kuzuia hivyo itawasaidia kupata uelewa mkubwa wa ugonjwa huo na taadhari zake. 


Awali akifungua mafunzo hayo Meneja wa Shirika la kutoa msaada wa kisheria mkoani Tanga (TAWOREC), Halima Saguti amesema, lengo la kutoa mafunzo kwa Paralegal hao ni kutaka wanapotoa huduma kwa wananchi huko vijijini waweze kujiinga na maambukizi ya ugonjwa huo. 


Amesema, kazi za wasaidizi hao wa kisheria zimekuwa zikiendelea huko vijijini na hivyo kupewa elimu hiyo kutasaidia kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo kwa watu wengine.