November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yaonya wanaofungia watoto wenye ulemavu

Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya

CHAMA cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Mbeya kimewaonya wazazi na walezi wanaowafungia ndani watoto wenye ulemavu na badala yake watoe ushirikiano wa kuwafichua ili waweze kuhesabiwa kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajia kuanza mwezi  Agost Mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa  mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti  wa CCM , Mkoa wa Mbeya,Mchungaji  Jacob Mwakasole wakati akizungumza na Times majira ofisini kwake kuhusu na utaratibu wa Serikali  kuwafikia watu walio katika kundi hilo miongoni mwa jamii.

Mchungaji Mwakasole amesema  kuwa tayari Serikali imetoa maelekezo kwa wa ngazi za Kata na vijiji kuhakikisha wanapita kutoa elimu kwa jamii na Wazazi wenye watoto walio na changamoto hiyo kuwafichua hadharani na si kuwaficha majumbani.

“Ukishapata mtoto mlemavu unakuwa umepewa  zawadi  kutoka  kwa Mungu ,kumficha ni dhambi kubwa sana hivyo lazima umshukuru kwasababu ukiwa na mlemavu   au asiye na ulemavu ni lazima useme asante Mungu  ,nawasihi wazazi wawe waadilifu  na waaminifu mbele za  Mungu  “amesema Mwenyekiti huyo.

Akizungumzia kuhusu watendaji ambao watapewa dhamana la kuhesabu watu Mwakasole amesema kwamba kiapo ambacho watapewa wakawe waaminifu  na asije akaonekana hata mmoja ambaye atakwenda kinyume na wakifanya hivyo watakuwa wamelikosea Taifa.

“Lakini kunapokuwepo na takwimu  za watu ndivyo hata serikali inajua jinsi gani inajiandaa katika masuala ya uchumi  unapojua idadi katika nchi yako  unapoanza kuandaa masuala ya uchumi kujua vituo vya afya vingapi elimu ,maji ,hapo ndo itakuwa rahisi sana kupata idadi ya watu wenye ulemavu hivyo suala la`Sensa ni muhimu sana”alisema Mwakasole.

Amesema CCM ,Mkoa wa Mbeya  umejipanga vizuri kwa   kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa zoezi la sensa ya` watu na makazi   kuwafikia watu hususani kundi kla watu wenye ulemavu .

Aidha ameongeza kuwa wamejipanga kuendelea kusisitiza serikali  na kuagiza serikali  kwa maana ya watenda ili waweze kuwafikia watu wote hasa kundi la watu wenye ulemavu  na kuhakikisha wote wanahesabu  kwa umakini .

Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Mkoa wa Mbeya ,Bashiru Madodi amesema viongozi wa mashina wahakikishe walemavu wote wahakikishe wanatolewa ndani na kuhesabiwa .

“Chama kwa utaratibu wetu huwa kunakuwa na maelekezo  maalum toka makao makuu ,tunachofanya sasa hivi tunahamisha viongozi wa mashina  hawa tunaamini ndo wanaishi na watu kila na kujua wa aina gani hivyo wahakikishe wanasimamia zoezi hili kikamilifu “amesema Madodi.

Rose Emmanuel ni mkazi Kabwe Jijini Mbeya amesema kwamba  zoezi hilo la` Sensa ya watu na makazi muhimu hivyo ni muhimu wazazi wakatoa ushirikiano kwa watendaji wa serikali ambao watakuwa kwenye zoezi hilo ili kundi la watu wenye ulemavu.

“Kwenye maeneo yetu tuna watu wazima na watoto ambao wapo ndani hivyo ni vema  zoezi  hili likaweza kuwafikia watu hawa na wazazi watoe ushirikiano kwa watendaji wakati wa zoezi hili ili watu wenye ulemavu waweze kuhesababiwa  katika maeneo yao”amesema Rose.