Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
SHIRIKA la Bima Zanzibar (ZIC) Februari 10 limekutana na kuzungumza na Mawakala na Madalali wa shirika hilo katika kikao kilichofanyika Hoteli ya Cate Jijini Dar es Salaam.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) Araf Haji amesema Mwaka huu wamejikita zaidi Katika kuboresha Huduma kwa wateja na kurahisisha upatikanaji wa Bima hasa kwa kujikita katika kutoa huduma kwa njia ya Mtandao.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Uongozi wa Shirika hilo ukiongozwa na Mkurugenzi huyo akiambatana na Meneja wa Kanda ya Pwani Majda Issa Ahmed na Ndugu, Mohammed Ameir Mkurugenzi Biashara (ZIC).
Aidha Haji amefafanua zaidi kuwa kikao hicho kimeazimia kuwa na Mategemeo ya kuboresha Mahusiano Mazuri kati ya Shirika hilo pamoja na Mawakala hao na kuongeza ukuaji wa Biashara.
“Tunategemea Mahusiano haya ambayo yamejengeka yataweza kusaidia kuboreshwa Kwa Huduma pamoja na changamoto zilizowasilishwa zitaweza kutatuliwa Kwa haraka na nawasihi muendelee kuwa mabalozi wazuri wa ZIC.”
Kwa upande wake Meneja wa Shirika hilo Sabri Ali amesema kikao hiko kimekuwa chenye Manufaa kutokana na Madalali hao kuwasilisha changamoto zao hivyo kama Shirika limeweza kufikishiwa changamoto hizo na kuahidi kuzitatua Ili kuleta ufanisi wa huduma Kwa wateja.
Sabri amesema Shirika lipo mbioni kuongeza huduma nyingine na Bima ya usafiri hasa usafiri kwa wasafiri waendao nje ya Tanzana pamoja na kuleta huduma ya bima ya Afya Kwa wateja wao ili kuwahakikishia wanapata huduma zilizo bora zaidi .
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili